Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara, akizungumza na Wahitimu wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), (hawapo pichani), kwenye mahafali ya 37 ya chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, Disemba 10, 2021.
Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara (kulia), akiwa ameambatana na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zakaria Mganilwa, Wakiwasili katika mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es salaam.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, Prof Zakaria Mganilwa, akitoa taarifa Kwa Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara (hayupo pichani) wakati wa mahafali ya 37 ya chuo hicho yaliyofanyika Jijini Dar es salaam,

Baadhi ya wahitimu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), wakimsikiliza Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara,(hayupo pichani), wakati akihutubia kwenye mahafali ya 37 ya chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, Disemba 10, 2021.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, (wa katikati), akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), kwenye mahafali ya 37 ya chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, Disemba 10, 2021.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara(kushoto), akizungumza na Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT), Prof. Zakaria Mganilwa wakati wa Mahafali ya 37 ya chuo hicho, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, Disemba 10, 2021.


Naibu Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, Mhe. Mwita Waitara, akiwa katika picha ya pamoja na wahitimu wa kozi ya uhudumu ndani ya ndege (cabin crew), wakati wa Mahafali ya 37 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji, yaliyofanyika Jijini Dar es salaam, Disemba 10, 2021.

Na Karama Kenyunko Michuzi TV 
SERIKALI imewataka wanafunzi wanaendelea na masomo kuwa wabunifu na kusoma kwa bidii ili pindi wanapomaliza masomo yao waweze kuwa na maarifa na ujuzi wa kutosha utakaowawezesha kujiajiri ama kuajiliwa.

Hayo yamesemwa leo Desemba 10,2021  jijini Dar es Salaam na Naibu Waziri Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, Mwita Waitara wakati wa mahafali ya 37 ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) yaliyofanyika katika viwanja vya Chuo hicho.

"Katika zama hizi ambazo nchi yetu ipo katika uchumi wa kati, ubunifu ni jambo muhimu sana hasa katika kipindi hiki cha mabadiliko makubwa ya Teknolojia hivyo ubunifu utawezesha kujiajiri ama kuajiriwa ukizingatia Uchumi wa Viwanda unahitaji nguvu kazi yenye maarifa na ujuzi zaidi". Amesema Waitara

Amesema, idadi ya wahitimu ni ushahidi tosha kuwa Chuo kinafanya juhudi kubwa kuhakikisha wanakuwa na wataalam wa kutosha katika Sekta ya Uchukuzi hivyo pamoja na juhudi hizo, ametoa wito kwa Uongozi wa Chuo kuendelea kuwa wabunifu na kufanya kazi kwa bidii ili kukifanya Chuo hicho kuwa na mahali sahihi pa kujifunzia.

Aidha amesema Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi na Uchukuzi, inafahamu vizuri changamoto zinazokikabili chuo hicho ikiwa ni pamoja na uchakavu wa miundombinu na majengo, uhaba wa ofisi za wahadhiri na uhaba wa nafasi za mabweni kwa wanafunzi.

Serikali kupitia Wizara ya Ujenzina Uchukuzi, inafahamu vizuri changamoto zinazokikabili Chuo ikiwa ni pamoja na uchakavu wa Miundombinu na majengo, uhaba wa ofisi za wahadhiri na uhaba wa nafasi za mabweni kwa wanafunzi, hata hivyo, serikali itaendelea kushirikiana na Chuo katika kuhakikisha changamoto hizi zinapatiwa ufumbuzi.

"Ninauagiza Uongozi wa Chuo kuendelea kutumia mapato ya ndani katika kuendeleza na kuboresha miundombinu ya Chuo,” amesema Waitara.

"Wahitimu hawa ni matunda ya kazi yenu nzuri, kwa hiyo dumisheni na kulinda jitihada hizi katika kufikia malengo ya kuwapata wahitimu bora kwa mahitaji ya nchi yetu. Bila ushirikiano wenu, Mahafali haya yasingekuwepo. Rai yangu kwa Wanataaluma ni kwamba ongezeni bidii katika kazi zenu kwa maendeleo endelevu ya Uchumi wa Viwanda. amesema.

Kwa upande wake, Mkuu wa Chuo cha NIT, Profesa Zacharia Mganilwa amesema idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa na chuo imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka hivyo kupelekea ongezeko la wataalam katika sekta ya uchukuzi.

“Katika kipindi cha miaka mitano idadi ya wanafunzi imeongezeka kwa asilimia 67 kutoka 7,752 mwaka 2016/2017 hadi wanafunzi 12,980 mwaka 2021/2022,” amesema.

Amesemw,  Chuo kina jumla ya wafanyakazi 346 ikiwa wanataaluma ni 224 na waendeshaji wapatao 122 idadi ambayo ni  ndogo hasa kwa wanataaluma ikilinganishwa na mahitaji halisi ya Chuo na hivyo kukilazimu chuo kutumia fedha nyingi kuwalipa wahadhiri wa muda ili kuziba upungufu uliopo. 

"Chuo chetu kina mikakati mbalimbali ya kutayarisha Rasilimali Watu watakaokidhi mahitaji ya soko la ajira kwenye sekta ya Uchukuzi na Usafirishaji hasa kwa kuzingatia utekelezaji wa mageuzi makubwa ya kiuchumi ambayo  Serikali ya Awamu ya sita imendelea kuyafanya.

"Tutaanzisha na kuhuisha mitaala mbalimbali kuanzia ngazi ya stashahada hadi shahada ya uzamili ikiwa ni uboresha mazingira ya kufundishia na kujifunzia hii ikiwa ni ukarabati na ujenzi wa majengo mapya, ununuzi wa vifaa vya maabara na karakana" amesema.

Amesema Chuo pia katika kuimarisha utoaji wa mafunzo kwa wataalam mbalimbali, kimeanzisha Kituo cha Umahiri cha Mafunzo ya Taaluma za Anga na Operesheni za Usafirishaji (Center of Excellence in Aviation and Transport Operations - CoEATO) kwa mkopo kutoka Benki ya Dunia ambapo  Fedha hizo zitatumika kujenga madarasa, maabara, karakana pamoja na kununua vifaa vya mafunzo ikiwemo, Cabin Crew Mock Up, Aircraft Runnable Engines, Flight Simulators naVirtual Maintenance Trainers.

"Hadi sasa, Chuo kimeanunua Cabin Crew Mock Upaina ya Boeing 737 – 800 kwa ajili ya mafunzo ya wahudumu wa ndani ya ndege ambayo inavifaa vinne ikiwemo Fixed Cabin Emergence Evacuation Trainer, Ditching Trainer, Fire Fighting Trainer pamojana Door trainer. Vifaa hivi kitaopokelwa mwezi Januari, 2022", amesema.

Ameongeza kuwa katika maandalizi ya mafunzo ya urubani, chuo kimepeleka wafanyakazi wanne nchini Afrika ya Kusini kusomea urubani na ukufunzi wa mafunzo ya urubani katika vyuo viwili ambapo wafanyakazi wawili wapo Blue Chip Flight School na wengine wawili wapo 43 Air school

Naye,  Profesa Blasius Nyichomba, Mwenyekiti wa baraza la uongozi wa chuo hicho,  amesema baraza hilo la uongozi limefanikiwa kusimamia uboreshaji wa miundombinu na mazingira ya kufundishia nakujifunzia, uboreshaji wa mafunzo yanayotolewa na chuo, pamoja na kuimarisha rasilimali watu ya chuo.

“Usimamizi huu unalenga kukiwezesha chuo kufikia malengo ya uanzishwaji wake, ili kuchochea maendeleo ya Taifa ya uchumi kama yalivyoainishwa kwenye Dira ya Taifa ya Maendeleo ya Mwaka amesema.

Ameongeza kuwa Chuo kimeanza kutekeleza  Mpango Mkakati wa Miaka Mitano mwaka2020/21 – 2025/26, ambato ndio Dira ya Chuo katika utekelezaji wa majukumu yake.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...