Na Amiri Kilagalila, Njombe
MUHITIMU wa darasa la saba mwaka huu mkazi mtaa wa uhuru kata ya Maguvani halmashauri ya mji Makambako mkoani Njombe mara baada ya kuonywa kuhusu upotevu wa fedha katika duka la baba yake.
Mtoto huyo amekutwa amejinyonga eneo la jikoni kwa kutumia kamba ya manila.
Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Njombe Hamis Issah alisema limetokea disemba moja majira saa tatu huko Makambako.
Kamanda amesema kwamba mtoto huyo baada ya kumaliza mtihani wa darasa la saba baba yale alimuachia duka akawa anauza eneo la sokoni Makambako.
"Kilichotokea cha ajabu ni kwamba baba katika kuangalia mahesabu ya duka aliona hayaendi vizuri na usiku wa tarehe moja alimuonya mtoto huyo kwamba kama anachukua pesa hizi usiendelee kuzichukua"alieleza Kamanda.
Kamanda amesema"Mtoto huyu kitendo kile kilimkasirisha na matokeo yake akachukua maamuzi ya kujinyonga na amekutwa asubuhi ya tarehe mbili akiwa amejinyonga eneo la jikoni kwa kutumia kamba ya manila.Dada yake alimuona na alitumia kisu kukata hiyo kamba bila ya mafanikio yoyote kwa sababu alikua anataka kumuokoa ndugu yake na walivyokua wakimkimbiza hospitali ya nazalet iliyopo hapa hapa Makambako mtoto huyu alifariki dunia"alisema Kamanda.
"Ni mtoto ambaye alitegemea kwenda kidato cha kwanza mwaka kesho alimalimaza darasa la saba hivi karibuni maana kijana kama huyu kuchukua maamuzi ya kujinyonga nae ni kijana ambaye ndoto zake za baadae naona leo zimepotea,zimefika mwisho"alisema Kamanda Issah.
Pia kamanda Issah ametoa wito kwa wananchi na watoto na wazazi kwenda taratibu na watoto huku akielezwa kwamba na vijana mmomonyoko wa maadili umekua sio mzuri katika jamii.
Wakati huo huo mtu mmoja ambaye ajajulikana anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 60 amekutwa amejinyonga kwa kutumia kamba ya mti ndani ya msitu wa miti ya kupandwa huko katika kijiji Ikando kata ya Kichiwa wilayani Njombe.
Tukio hilo limetokea tarehe mbili majira ya saa 12 jioni huko kijiji cha Ikando.
Pia aliwataka vingozi wa dini,viongozi wa mila taasisi mbalimbali kutoa elimu na kukemea maamuzi ya watu kujichukulia sheria mikononi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...