KAMPUNI ya Nkusu Theo Sugar Limited (NTS) yenye  Makao yake Makuu Mkoani Mbeya inatarajia kujenga kiwanda sukari mkoani Ruvuma chenye uwezo wa kuzalisha tani 120,000 mwaka ili kukabiliana na changamoto ya upatikanaji wa bidhaa hiyo, huku ujenzi wake ukinatarajiwa kuanza mwakani katika kijiji cha Nakawale katika Halmshauri ya wilaya ya  Songea baada ya kupatiwa hati miliki ya ardhi ya eneo hilo.

Afisa Mkuu wa Fedha Na Utawala wa Kampuni hiyo Bwana Longinus Kagaruki amesema tayari tani 50 za mbegu za miwa zimeanza kuzalishwa na heka 50 za mashamba ya miwa wanatarajia kupanda, ambapo mwisho  wa mwaka huu Wizara ya Ardhi wanatarajia kutoa hati miliki.

Aidha Bwana Kagaruki ameongeza kuwa kiwanda hicho kitakuwa ni kiwanda cha pekee hapa Tanzania kwani licha ya kuzalisha sukari nyeupe ya viwandani na ya matumizi ya kawaida, bidhaa nyingine zitazalishwa kutokana na mabaki ya miwa ikiwemo,umeme megawati 432,mbolea na ethanol ambazo zitauzwa ndani na nje ya nchi.  Vilevile ajira 20,000 zinatarajiwa kuzalishwa.

“Kwa kweli hiki kitakuwa kiwanda cha pekee sana hapa Tanzania licha ya kuzalisha tani 120,000 za sukari kwa mwaka hakuna mabaki  yatokanayo na miwa yatakayotupwa kwani yatatoa product nyingine” alisema.

Pia kampuni itatoa fursa kwa wananchi wa kijiji cha Nakawale (outgrowers) kulima  miwa na kuuza kiwandani hapo ili kuwa na utoshelevu, ambapo Bodi ya Sukari Tanzania wamekubali kutoa mbegu kwa wakulima ili kuhakikisha kila mwaka sukari inapatiakana ya kutosha.

 Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Songea Bwana Menas Komba amesema kwa kuwa wananchi na viongozi wa Serikali Mkoani Ruvuma wamekubali na kutoa eneo kwa ajili ya ujenzi wa kiwanda hicho ameziiomba Mamlaka zote kuhakikisha wanaisaidia Kampuni hii upatikanaji wa hati miliki ili ujenzi wa kiwanda uanze kwani wananchi wanakiu kwani kitakuza uchumi,ajira na pato la mtu mmoja mmoja .

Aidha Bwana Komba ameongeza kuwa kujengwa kwa kiwanda hicho kutapunguza upungufu wa sukari na mbolea ndani ya mkoa wa Ruvuma na Tanzania kwa ujumla pia kupunguza uagizaji wa sukari toka nje.

“Niombe Serikali iendelee kufanya haraka kukupatia hiyo hati miliki  sababu sisi wenye eneo tumeshakubali na halina mgogoro wowote.

 Na katika Halmshauri yetu tuna maeneo mazuri mabonde makubwa  yenye maji mengi tunawakaribisha kwani hatuna urasimu ”alisema

Katika hatua nyingine Kampuni ya Nkusu Theo Sugar Ltd imetoa msaada wa vifaa vya ujenzi ambavyo ni nondo ,rangi, nyaya pamoja mifuko mia moja, ya saruji kwa ajili ya kwenda kumalizia vyumba viwili vya madarasa yaliyojengwa kwa nguvu za wananchi katika shule ya msingi Nakawale kama sehemu ya kutambua mchango wa wananchi katika uwekezaji huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...