Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali: -
1. Amemteua Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wa Awamu ya Nne Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita (06) kuanzia tarehe 17 Januari, 2022.
2. Amemteua Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR). Balozi Mwinyi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
3. Amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre (AICC). Balozi Taji ni Balozi Mstaafu wa Tanzania, Paris nchini Ufaransa
Teuzi hizi zimeanza tarehe 28 Desemba, 2021.
4.
Amemteua Bw. Patience
Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala
Bora. Bw. Ntwina alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Katiba na ufuatiliaji wa Haki kutoka
Wizara ya Katiba na Sheria.
Uteuzi huu umeanza tarehe 30 Desemba, 2021.
Jaffar Haniu
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, Ikulu.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...