NA YEREMIAS NGERANGERA….SONGEA.
Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali Wilbert Ibuge aliyasema hayo katika kikao cha baraza la maendeleo ya mkoa, kuwa mkoa wa Ruvuma ni imara na utaendelea kuwa imara katika Nyanja ya ulinzi na usalama ,kiuchumi,kielimu pamoja sekta ya afya.
Brigedia Generali Ibuge alidai mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa na uchumi imara kutokana na wananchi wa mkoa wa Ruvuma kuendelea kuzalisha mazao ya kilimo kwa wingi na kuufanya mkoa kupata chakula cha kutosha na ziada kwa ajili ya biashara.
Aidha Mkuu wa mkoa aliongeza kuwa mkoa wa Ruvuma uliendesha mfumo wa mauzo kwa njia ya stakabadhi ghalani hali iliyowezesha wananchi wa mkoa wa Ruvuma kupata fedha kutokana na mauzo ya mazao yao kwa wakati .
Hata hivyo alisema Mkoa umeendelea kusimamia ujenzi wa madarasa 500 ya shule za msingi na sekondari ambapo ifikapo januari 2022 wanafunzi wa kidato cha kwanza na darasa la kwanza wapate madarasa ya kusomea.
Upande wa afya Mkuu wa mkoa wa Ruvuma alikiambia kikao cha baraza kuwa mkoa unatarajia kujenga hospitali ya mkoa wa Ruvuma katika eneo la Mwenge mshindo lililopo manispaa ya Songea ili kuongeza utoaji wa huduma za afya kwa wananchi wa mkoa wa Ruvuma.
Awali Mkuu wa mkoa wa Ruvuma alikiomba kikao cha baraza la maendeleo ya mkoa kutumia kikao hicho kwa umoja wao kuwaomba viongozi wa dini kuomba mvua ili wananchi wa Mkoa wa Ruvuma ambao shughuli yao kubwa ni kilimo inategemea mvua .
Mchungaji wa kanisa la Morovian Suleimani Wilson Nziaba na Shekh Musa Ponera waliomba sala na dua ya kuomba mvua katika nchi yetu ili wananchi wa mkoa wa Ruvuma ambao wanategemea kilimo waweze kulima na kuzalisha mazao kama miaka mingine.
Mkoa wa Ruvuma una jumla ya wilaya tano ambazo ni Tunduru,Mbinga,Namtumbo,Songea na Nyasa huku kukiwa na Halmashauri nane ambazo ni Mbinga mji,Halmashauri ya Mbinga,Manispaa ya Songea,Halmashauri ya Songea,Madaba,Namtumbo,Tunduru na Nyasa ambapo mpaka sasa mkoa wa Ruvuma umeendelea kuwa imara .
Pcha ya wajumbe wa kikao cha baraza maendeleo ya mkoa wa Ruvuma wakiwa katika maombi ya kuomba mvua kilichofanyika katika ukumbi wa manispaa songea
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...