Na Khadija Kalili Kibaha
Mkuu wa Mkoa wa Pwani Alhaj Abubakar Kunenge  amesema mwaka huu kuna mabadiliko makubwa kwa zao la Korosho kutokana na ubora wake ikilinganishwa na ilivyokuwa  mwaka Jana.

"Mwaka  jana Mkoa wa Pwani ulikua na changamoto ya kuzalisha Korosho zenye ubora  wa daraja la kwanza  tofauti na ilivyo kwa mwaka huu ambapo bei ya wastani ilikua 1300 kwa kilo moja kwa Korosho za daraja la kwanza lakini  mwaka huu bei imepanda hadi kilo moja imenunuliwa kwa Sh. 2,400 hivyo imekua ni faida kwa mkulima.

RC Kunenge alisema hayo leo alipokuwa alifanya ziara ya kutembelea viwanda vinavyobangua Korosho  vilivyopo Wilayani Kibaha Mkoa wa Pwani.
Akiwa  katika Kiwanda Cha Tera Cashew nuts kilichopo eneo la Tanita Kibaha alisema kuwa Mkoa  utahakikisha matarajio ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan yanafikiwa  kwa kubangua Korosho ndani ya Mkoa wa Pwani ambapo  ubanguaji utafanyika kwa  njia za kisasa kiwandani hapo.

"Tutahakikisha Korosho zote zinakuja kubanguliwa Mkoa wa Pwani na hata zinazotoka nje ya Mkoa huu  tutahakikish tunafikia hili tamanio la Mheshimiwa Rais alilolisema hivi karibuni kuwa anataka kuona Korosho zinabanguliwa ndani ya Mkoa wetu  tutatimiza hilo kwa ufanisi  mkubwa kwani hivi Sasa ubora wa korosho umeongezeka"alisema RC Kunenge
Aidha mbali ya Kiwanda Cha Tera Cashew nuts pia alitembelea Kiwanda Uvuki kilichopo Visiga Kibaha.
"Tumetembea Ili kuona uwezo wa ubanguaji wa zao  la Korosho ambapo Tera Cashew nuts uwezo wao ni mkubwa katika kubangua Korosho na kuzikausha Kisasa zaidi ambapo hubangua na kusindika tani 3000 kwa mwaka na pia wamesema kuwa wanatarajia  kuleta mashine nyingine mpya ambapo kwa siku watakuwa na uwezo wa kuzalisha tani 7 na kwa mwezi watazalisha   tani  zaidi ya 200, kama mlivyoona kuwa kiwanda Tera Cashew nuts ni Kiwanda kikubwa cha ubanguaji korosho  katika Mkoa wa Pwani na nchini kwa ujumla.

Meneja wa Kiwanda hicho Chiraq Patel alisema  kuwa Tera Cashew nuts  wanauza  Korosho katika soko la nje  huku alizitaja baadhi ya nchi wanazouza kuwa ni Morocco, Ethiopia, Hispania 

Mwaka jana Mkoa wa Pwani  ulizalisha tani 7,000 tu na mwaka huu  tayari asilimia 77 ya Korosho ni nidaraja la kwanza hivyo zimeongezeka ubora wake.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...