Baadhi ya washiriki wa Mahafali ya kukabidhi vyeti vya umahiri kwa mafundiwa vifaa vya mawasiliano mkoani arusha,wakiwa katika picha ya pamoja na mgeni rasmi Kamanda wa Jeshi la polisi mkoa wa Arusha Jastine Masejo 7/12/2021,lMhandisi msaidizi Kadaya Baluhye (TCRA)kwenye mahafali ya kukabidhi vyeti vya umahiri kwa mafundiwa vifaa vya mawasiliano mkoani Arusha,kulia kwake ni kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Justine MasejoKamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Arusha Jastine Masejo,akizungumza katika mahafali ya kukabidhiwa vyeti vya umahiri kwa mafundi wa vifaa vya huduma ya mawasiliano iliyofanyika leo mkoani Arusha katika ukumbi wa Golden Rose hotelKamanda wa polisi Mkoani Arusha Justine Masejo kukabidhi cheti cha umahiri kwa mmoja wa fundi wa vifaa vya mawasiliano ambapo hafla hiyo ilifanyika katika hoteli ya Golden Rose Mkoani Arusha.


Na.Vero Ignatus,Arusha

Watumiaji wa huduma za mawasiliano wanazo haki mbalimbali ambazo zinawapa ulinzi wanapotumia huduma na bidhaa hizo,ambapo haki hizo zimeainishwa kwenye kanuni za kulinda watumiaji zinazotokana na matumizi ,bidhaa husika,masharti ya leseni za watoa huduma au kwa mujibu wa matakwa ya sheria husika

Ameyasema hayo  Mhandisi msaidizi Kadaya Baluhye (TCRA)kwenye mahafali ya kukabidhi vyeti vya umahiri kwa mafundiwa vifaa vya mawasiliano mkoani Arusha, kuwa watumiaji pia anayo haki na wajibu unaompasa kuzingatia ,kuhusu huduma wanazotarajia kujiunga nazo na zile zinazotolewa kwao.

Baluhye amesema (TCRA) wataendelea kushirikiana na Umoja wa mafundi simu  (UMSA ) Mkoa wa Arusha, kwa kutoa mafunzo ya mara kwa mara ili kuboresha utendaji kazi wao,ambapo  aliwasisitiza kuwa, kama wanahitaji kuwa na ufundi stadi lazima watambulike na serikali ili Mamlaka iwatambue ili wawe mikono salama

Pia, mwakilishi wa mafunzo stadi  vyeta Charles Mapuli Mratibu wa mafunzo kutoka Veta amesema kwa kushirikiana na veta, TCRA na DIT ,wataweza kupanua wigo wa mafunzo kwa kundi kubwa la vijana ambao ni mafundi simu.

Akisoma risala kwa niaba ya mafundi Nasri Mshana mwenyekiti wa umoja wa mafundi simu mkoa wa Arusha , amesema kuwa kwa sasa wana mafundi mahiri wenye ujuzi wa simu za viganjani,hivyo wananchi wasisite kuwatumia katika matengenezo ya vifaa vyao vya Mawasiliano.

Anasema awali taaluma hiyo ilikuwa inafanyika kiholela, japo kuwa simu za kiganjani ni kazi ngumu kwani zimekuwa zikifanyakazi ambazo zinfanywa na kopyuta, kwani ni kifaa muhimu kwa Maisha ya binadamu

Simu hizi zikitumika vyema zitaleta manufaa makubwa kwa watu ,lakini ikitumika vibaya ni zaidi ya bomu la atomiki ,kwa kushirikiana kwa pamoja lengo la serikali litatimia alisema Nasri

Mgeni rasmi katika halfa hiyo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha ACP. Justine Masenjo  aliwataka mafundi simu hao  waliohitimu zaidi ya 100 ,kutumia mafunzo hayo kama chachu ya kukuza weledi wao, katika fani ya matumizi ya vifaa vya  mawasiliano na uaminifu bila kusahau usiri juu ya kifaa Cha mteja .

Masejo amesema, kumekuwa na wimbi la wizi wa simu na hupelekwa kwa mafundi simu kwa ajili ya kufuta data za simu iliyoibiwa, limeshamiri na kuwataka mafundi simu waliohudhuria mafunzo hayo kuwa mabalozi katika mapambano dhidi ya watu  wanachafua taswira safi ya mafundi simu .

Amesema Jeshi la Polisi Mkoa wa Arusha linaendelea na operesheni ya ukamataji wa mafundi simu ambao wanaenda kinyume na maadili ya kazi hiyo.

Bila sekta ya teknolojia na Habari nchi haiwezi kuendelea hivyo lazima kila fundi awe na weledi wa kutosha kwani jamii imewaamini na kuwapelekea vifaa vyao hivyo jengeni uaminifu na usiri.Alisema Kamanda

Amewataka kutokuridhika na mafunzo hayo bali wajiendeleze zidi kwani teknolojia inakwenda inabadilika kwa kasi sana hivyo ni vyema kujiongeza kila mara kwani wanao mchango mkubwa katika taifa

Nao baadhi ya wahitimu wa mafunzo hayo wameshukuru Mamlaka ya Mawasiliano TCRA, VETA, DIT  kwa kuwapa mafunzo ambayo yamewaongezea ujuzi zaidi katika kazi zao.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...