Na Amiri Kilagalila,Njombe

Mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya,amewaagiza wakandarasi kutekeleza miradi ya maji kwa ubora na kuzingatia viwango ili kuwasaidia wananchi wa mkoa huo kuweza kupata maji kwa uhakika.

Rubirya ametoa maagizo hayo mara baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikataba mitano ya maji yenye thamani ya zaidi ya bilioni tatu baina ya Wakala ya Usambazaji Maji na Usafi wa Mazingira (RUWASA) mkoa wa Njombe na wakandarasi uliofanyika katika ukumbi wa NSSF mjini Njombe.

“Hali ya upatikanaji wa maji katika mkoa wetu bado ni asilimia 75 na hii asilimia bado inachangamoto zake nyingi,kuna maeneo maji yanakatika lakini kuna maeneo maji yanatoka ni machafu lakini tunayo miradi mingi ambayo utekelezaji wake umechukua muda mrefu sana”alisema Rubirya

Rubirya ameagiza kuwa “Sasa hivi mmesaini mikataba hapa mitano ambapo zaidi ya Shilingi bilioni tatu na milioni mia tatu na nne zitatumika kuendeleza miradi hii.Niwaelekeze makandarasi mhakikishe kuwa mnakwenda kutekeleza miradi hii kwa ubora unaotakiwa na kwa kuzingatia viwango ambavyo vinaelekezwa katika miradi hii”

Mhandisi Wilson Novath ni kaimu meneja kutoka RUWASA mkoa wa Njombe amesema miongoni mwa miradi inayokwenda kutekelezwa ni pamoja na miradi miwili iliyopo wilayani Makete itakayowanufaisha wakazi 3760,mradi mmoja katika halmashauri ya wilaya ya Njombe uliopo kijiji cha Nyombo utakaonufaisha wakazi 3515 huku miradi mingine ikiwa katika wilaya zingine za mkoa huo wa Njombe.

Aidha amesema upatikanaji wa maji mjini umefikia 69.3% huku vijijini ukiwa 78.6% . na hivyo utiaji saini wa mikataba hiyo unakwenda kuongeza chachu katika zoezi la usambazaji maji na kumtua ndoo ya maji mama kichwani

“Upatikanaji wa maji kwa wilaya ya Njombe ni 67%,Makambako ni 59.1%,Wanging’ombe 81%,Makete 82.7% na halmasahuri ya wilaya ya Ludewa 46.0%”amesema Mhandisi Novath.
Kulia ni mhandisi kutoka RUWASA pamoja na moja ya wakandarasi kushoto wakisaini mkataba wa utekelezaji wa miongoni mwa miradi inayokwenda kutekelezwa mkoani Njombe.
Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akizungumza mara baada ya kushuhudia zoezi la utiaji wa saini katika mikataba ya miradi ya maji.
Mkuu wa mkoa wa Njombe mhandisi Marwa Rubirya akishuhudia zoezi la utiaji saini mikataba ya uetekelezaji wa miradi ya maji.

Baadhi ya mikataba ikionekana mbele ya wataalamu kabla ya zoezi la utiaji saini lililofanyika mjini Njombe.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...