SBL yaungana na mataifa mengine duniani kuadhimisha siku ya kimataifa ya watu wenye ulemavu inayoadhimishwa kila mwaka tarehe 3 Desemba.
Siku hii inalenga kudumisha usawa na ustawi wa watu wenye ulemavu katika kila ngazi ya jamii na maendeleo, na kuongeza ufahamu kuhusu watu wenye ulemavu katika nyanja zote za maisha ya kisiasa, kijamii, kiuchumi na kitamaduni.
SBL ikiwa mmoja wa wadau wakubwa mnamo tarehe 26 Novemba ilimulika jengo la makao yake makuu kwa rangi ya zambarau ikiwa miongoni mwa mfululizo wa shughuli za kuadhimisha siku hiyo.
Kauli mbiu ya siku ya walemavu duniani ni "Uongozi na ushiriki endelevu kwa watu wenye ulemavu duniani baada ya COVID19 ''.

Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...