Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa na waziri wa mambo ya ndani, George Simachawene wakifungua pazia kuashiria uzinduzi wa Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mtumba Jijini Dodoma, chenye hadhi ya Daraja A ambapo Ujenzi wake utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 948 hadi kukamilika kwake.
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa Majaliwa akizungumza wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mtumba Jijini Dodoma, chenye hadhi ya Daraja A ambapo Ujenzi wake utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 948 hadi kukamilika kwake.

SERIKALI imesema itaendelea kuboresha na kujenga majengo mbalimbali ikiwemo majengo ya kutolea huduma ya Jeshi la Polisi nchini pamoja na jitihada mbalimbali zinazoendelea kufanyika ikiwa ni mafanikio ya Uhuru.

Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa wakati wa hafla ya kuweka Jiwe la Msingi kwenye Mradi wa Ujenzi wa Kituo cha Polisi Mtumba Jijini Dodoma, chenye hadhi ya Daraja A ambapo Ujenzi wake utagharimu kiasi cha shilingi Milioni 948 hadi kukamilika kwake.

Kwa upande wake Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini IGP Simon Sirro amesema Jeshi la Polisi litaendela kutimiza wajibu wake kwa kuhakikisha nchi inakuwa salama na Watanzania wanaishi kwa amani na utulivu bila kutishwa na mtu yeyote.

Aidha, IGP Sirro amesema kuwa fedha zinazotolewa na serikali zitaendelea kutumika vizuri kwenye miradi iliyokusudiwa ili kuwa na majengo bora na ya kisasa.

Akizungumzia kuhusu kituo hicho Mkuu wa kikosi cha Ujenzi cha Jeshi la Polisi, Mhandisi Fadhili Ishikazoba amesema kuwa, ujenzi wa kituo cha Polisi Mtumba ulianza tangu mwezi Julai mwaka huu na umepangwa kukamilika kwa muda wa miezi tisa na kwamba hadi sasa ujenzi huo umefikia asilimia 60 na unatarajiwa kutumia kiasi cha shilingi milioni 948 hadi kukamilika kwake na ukiwa unatekelezwa kwa mfumo wa Nguvu Kazi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...