Na Amiri Kilagalila,Njombe
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde, amesema serikali haitaweza kuivumilia halmashauri au kiongozi yeyote ambaye atashindwa kukabidhi kwa wakati ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa sababu imeshamthibitishia Rais Samia Suluhu Hassan kuwa madarasa elfu kumi na tano yanayojengwa nchi nzima yatakamilika kwa asilimia 100 ifikapo Desemba 30, mwaka huu.
“Hatutakuwa tayari na wala hatutamvumilia mtu yeyote ambaye atashindwa kumaliza haya majengo kwa wakati,hatutakubali kwasababu tumemthibitishia Rais”alisema Silinde
Msisitizo huo kutoka kwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais-Tamisemi, umetolewa mbele ya viongozi wa serikali wilayani Njombe sambamba na wakurugenzi wa halmashauri tatu za wilaya ya Njombe alipofanya ukaguzi wa utekelezaji wa ujenzi wa vyumba vya madarasa unaoendelea kutekelezwa tayari kwa maandalizi ya kuwapokea wanafunzi watakaoanza muhura mpya wa masomo ifikapo Januari mwaka 2022.
“Majengo elfu 15,000 yatajengwa ndani ya miezi miwili yakiwa yamekamilika kwa ubora,kwa viwango,na thamani halisi”alisema Silinde
Akiwa amefanya ukaguzi wa kuona kasi ya ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwenye halmashauri ya Mji Njombe, Halmashauri ya Wilaya ya Njombe na Halmashauri ya Mji Makambako, Mheshimiwa Lusinde hakusita kutoa pongezi kwa baadhi ya wakurugenzi waliosimamia vyema ujenzi wa vyumba hivyo hadi sasa.
“Pale Sovi ujenzi wa madarasa matano umakamilika kwa viwango vyenye ubora unaostahili”alisema Lusinde
Awali Naibu Waziri huyo akiwa ofisini kwa mkuu wa mkoa wa Njombe, amehakikishiwa na mkuu wa mkoa wa Njombe Mhandisi Marwa Rubirya, jumla ya vyumba 192 tayari vimejengwa kwenye mkoa mzima hadi sasa.
“Ujenzi umekamilika tunaendelea na ukamilishaji na kuna vyumba ambavyo vimekamilika kabisa na hata kesho watoto wanaweza wakahamia,na tumekubaliana kabla ya tarehe 25 madarasa haya niwe nimekabidhiwa”Alisema Marwa Rubirya
Naibu waziri ofisi ya Rais TAMISEMI David Silinde akikagua moja ya madarasa yanayoendelea kujengwa katika halmashauri ya mji wa Njombe.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...