Wenyeji na wageni wanaotarajiwa kutembelea mkoa wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa ajili ya mapunziko ya mwisho wa mwaka wameandaliwa burudani mbalimbali kwenye Tamasha kubwa linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro’ linalotarajiwa kufanyika tarehe 26 Desemba, 2021 katika Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka na Marangu hotel, mkoani Kilimanjaro.



Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mratibu wa Tamasha hilo kutoka Kampuni ya Real PR Solutions Bi Irene Lyimo alisema tamasha hilo ni sehemu ya mkakati wa kufanikisha mpango wa kuendeleza utalii wa ndani na linatarajiwa kupambwa na matukio mbalimbali ikiwemo maonesho ya Utalii na Biashara, Burudani na viburudisho mbalimbali ikiwemo vyakula vya asili michezo ya watoto pamoja na muziki tamasha hilo linatarajiwa kuhusisha Mbio za kujifurahisha.

“Mbio hizo zitahusisha Km 5, Km 10 na zinazotarajiwa kuanza majira ya saa 12:00 asubuhi.’’

“Aidha, siku tatu kabla ya mashindano hayo (tarehe 23 Desemba) kutakuwa na zoezi la kutoa misaada mbalimbali kwenye huduma za afya kibosho na Marangu, na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ambaye pia atawaongoza wafanyakazi wa umma, viongozi mbalimbali pamoja na wananchi, kutoa misaada kwenye hospital zetu.’’ Alisema.

Aidha, Bi Lyimo aliwaomba wakazi wa Mkoa wa Kilimajaro na mikoa jirani pamoja na wale wanaotarajia kwenda mkoani humo kwa ajili ya sherehe za mwisho wa mwaka kushiriki katika matukio hayo.

“Pia tunatumia fursa hii kuwaomba wafanyakazi pamoja na watumishi wengine katika mikoa hiyo kujisajili katika mbio hizo pamoja na shughuli nyingine zinazoambatana na tamasha hili la Twenzetu Kilimanjaro mwaka 2021 ikiwemo utoaji msaada katika hospitali zetu.’’ Alisema.

Akizungumzia zaidi kuhusu mbio za Capital Mountain Run zinazapamba tamasha hilo, Mtaalamu wa mbio wa mbio hizo Bw Joshua Kayombo alisema kwa kuwa tamasha hilo linalenga kutangaza utalii ili kuunga mkono jitihada za Rais Samia Suluhu Hassani, njia zitazatumika katika mbio hizo zinahusisha maeneo yenye vivutio ili kutoa fursa kwa washiriki kupata fursa ya kujionea mandhari nzuri za asili katika mkoa huo.

“Mbio hizi zitafanyika kwa wakati mmoja katika maeneo mawili tofauti yaani Marangu hotel na Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka kilichopo Kibosho. Baada ya mbio hizi washiriki watapata fursa ya kuendelea na burudani mbalimbali kwa ajili yao na familia zao ikiwemo vyakula vya asili, ngoma za asili na vinywaji mbalimbali,’’.

Akizungumzia kuhusu usafiri wa kuelekea kwenye tamasha hilo kutokea jijini Dar es Salaam na kurudi, Mkurugenzi wa Kampuni inayotoa huduma za usafiri wa abiria ya Wonderland Afrika Bw Bw Saidi Rukemo alisema wamejipanga kuhakikisha washiriki wanapata usafiri wa uhakika kwa bei nafuu kuanzia Disemba 24 na kurudi Disemba 27 baada ya tukio hilo.



Mratibu wa Tamasha laTwenzetu Kilimanjaro Bi Irene Lyimo (Kulia) sambamba na Mtaalamu wa mbio zitakazopamba tamasha hilo zinazofahamika kama Capital Mountain Run Bw Joshua Kayombo (Katikati) pamoja na muwakilishi wa wadau wa mbio hizo kutoka kampuni ya matangazo ya A1 Outdoor Bi Cassandra James (Kushoto) wakionesha medali na fulana maalum zitazotolewa kwa washiriki wa mbio hizo zinazotaraji wakufanyika tarehe 26 Desemba, 2021 katika Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka na Marangu hotel mkoani Kilimanjaro zikilenga kutangaza utalii wa ndani.



Mratibu wa Tamasha laTwenzetu Kilimanjaro Bi Irene Lyimo (Katikati) sambamba na Mtaalamu wa mbio zitakazopamba tamasha hilo zinazofahamika kama Capital Mountain Run Bw Joshua Kayombo (Kulia) pamoja na muwakilishi wa wadau wa mbio hizo kutoka kampuni ya matangazo ya A1 Outdoor Bi Cassandra James (Kushoto) wakizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu ujio wa Tamasha kubwa linalojulikana kama ‘Twenzetu Kilimanjaro’ linalotarajiwa kufanyika tarehe 26 Desemba, 2021 katika Chuo Cha Usimamizi wa Wanyamapori Mweka na Marangu hotel, mkoani Kilimanjaro likilenga kutangaza utalii wa ndani


Akizungumzia kuhusu usafiri wa kuelekea kwenye tamasha hilo kutokea jijini Dar es Salaam na kurudi, Mkurugenzi wa Kampuni inayotoa huduma za usafiri wa abiria ya Wonderland Afrika Bw Bw Saidi Rukemo (katikati) alisema wamejipanga kuhakikisha washiriki wanapata usafiri wa uhakika kwa bei nafuu kuanzia Disemba 24 na kurudi Disemba 27 baada ya tukio hilo.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...