MPANGO wa Tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), awamu ya pili unaoendelea kusaidia kaya maskini umekuwa mkombozi kwa watu wengi hususani  wakinamama waliopo Vijijini na kurudisha matumaini yao ya kuendelea kuishi duniani bila ya kuwa na woga wa maisha.

Mpango huo wa Tasaf kwa kaya maskini katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi Vijijini ulianza mwaka 2014 kwa utambuzi huku  utoaji wa ruzuku ulianza Julai, 2015 kwa kaya 7,020 ambazo baadae zilipungua mpaka kufikia kaya 6,456.

Kaya hizo ambazo nyingi zilikuwa zinakabiliwa na matatizo ya mabalimbali ikiwemo kula mlo mmoja kwa siku usiokuwa na uhakika, watoto kukosa elimu, na kukosa makazi ya kudumu huku pia wakikosa vyoo bora hali iliyowafanya kuwa na maradhi mbalimbali iliwafanya waishi maisha ya wasiwasi yasiyokuwa na matumaini.

Baada ya kaya hizo kuingia katika mpango wa ruzuku za Tasaf kwa wanufaika, asilimia kubwa ya kaya hizo wamejikwamua kiuchumi na kuweza kupata mahitaji yote muhimu ambayo walikuwa wakiyahijati kwa muda mrefu bila mafanikio.

Haya hivyo, licha ya wanufaika hao kwa kiasi fulani kufanikiwa kujikwamua kiuchumi ambapo sasa wanaweza kupata chakula cha uhakika kwa milo mitatu kwa siku, makazi ya kudumu, kujiingiza katika ufugaji ikiwa pamoja kuanzisha biashara mbalimbali lakini bado hawaamini kama wanaweza kuendelea na maisha yao bila ya ruzuku za TASAF.

Akizungumza hivi karibuni na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari waliokuwa ziarani mkoani Kilimanjaro, Selina Marika (46) anayeishi kijiji cha Sango, katika kitongoji cha Kombe, Kata ya Kimochi mkoani humo amesema, alianza kupokea hela za Tasaf Mwaka 2015 kwa kiasi cha Sh. 28,000 ambazo alizitumia kwa mkulima mahindi, kununua mbegu na dawa za kupigia mahindi .

Amesema, kiasi hicho cha pesa kilikuwa kidogo sana hivyo baadae aliongezewa hela na kufikia Sh. 36,000.

Baada ya fedha hizo kuongezeka  ikawa sasa napeleka kidogo shambani halafu nikawa natoa kidogo napeleka kwenye ujenzi maana nilikuwa naishi kwenye nyumba ya tope ambayo Ilikuwa karibu inaniangukia.

Nilifanikiwa kujenga nyumba ndogo na kutoka kwenye nyumba hiyo baada ya kuzalisha faida na kuwalipa watoto ada za shule.

Nawashukuru sana Tasaf bila wao ningekuwa nimesombwa na mafuriko kwani nyumba niliyokuwa nikiishi ilishaanguka nikaiegemeza na miti, yaani watu walikuwa wakipita na kuniona baada ya mvua walikuwa wakinipa pole na kumshukuru mungu kuwa nimepona, ningekuwa nimeisha potea. Tasaf ndio mmeniokoa, mshukuriwe sana mngekuta sipo,  ningekuwa Mandaka kama mvua ingeendelea kunyesha amesema Marika. 

Hata hivyo, Marika anaiomba Tasaf kama wanaweza kuongezea  kidogo ruzuku ili apate mlango na madirisha ili ngo'mbe waache kuingia ndani kwake. 

Aidha amewaasa wenzake ambao nao wanapata Ruzuku ya Tasaf kuzitumia fedha hizo katika kujikwamua kiuchumi na siyo kwenda kulewa pombe  kwani  pombe inapunguza afya yako, unamaliza hela bila kujua ulipomalizia zinakufanya mpaka unasahau,  yaani kuna anaenda  kunywa pombe wakishaenda kunywa atahakikisha anakunywa mpaka aimalize ile hela mkononi. sana.

Naye, Rahel  Mpanda, mkazi wa kijiji cha Sango, katika kitongoji cha Kommbe, Kata ya Kimochi ni ni miongoni kwa wanufaika ambao wamefanikiwa kujikwamua katika maisha ya awali kutoka kutopata mlo hadi kuwa na uhakika wa chakula na nyumba ya kudumu ya kuishi.

Rahel ambaye ni nufaika anayeishi na virusi vya Ukimwi anasema,  ruzuku ya Tasaf imesaidia kurudisha matumaini ya maisha kwa kupata uhakika wa chakula kwa wakati.

Mbali ya kumuwezesha kupata chakula lakini pia imemsaidia kupata mifugo ya ng’ombe na mbuzi  ikiwa pamoja na kujiunga na Vikundi vya Kinamama wa Tasaf na kumuwezesha kujenga nyumba bora ya kuishi.

Pamoja na matumaini hayo lakini Rahel anaamini bila Tasaf atarudi kule kule alipotoka kabla ya mpango huo haujatekelezwa.

Mpango huu umenisaidia sana, umetutoa mbali na kutupatia matumaini mapya ya kuishi, hapo nyuma sikuwa na  natumaini lolote, nilikuwa najionea niko mpweke nilikosa matumaini kabisa, kwani nimeathirika, tasaf wamenipa matumaini ya maisha amesema Rahel.

Hata hivyo kama ilivyokuwa kwa wanufaika wengine, Rahel naye anaamini bila ruzuku ya Tasaf hawezi kuishi kama anavyoishi sasa pamoja na kuwa na uwezo wa kulima kilimo cha mahindi na maharage pamoja na kufuga mbuzi na kuku wa kienyeji.

Wasiwasi huo unatokana na wanufaika hao kutokuwa na elimu ya ujasiliamali ambayo ingeweza kuwapa elimu ya kufanya biashara zao kitaalam na kuweza kusimamia fedha zinazotokana na biashara, kilimo na ufugaji na kuwawezesha kuwakwamua zaidi ya walipo sasa.

Akizungumza baada ya kusikia kilio cha wanufaika hayo Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi Vijijini, Castory Msigala ameahidi kulifanyia kazi jambo hilo la kuwaongezea elimu wanufaika hao kwa lengo la kuwasaidia ili waweze kujitegemea na ruzuku zao ziende kwa wanufaika wengine.

Msigala amesema amesikia maombi ya wadau mbalimbali ya Tasaf ikiwa kupata elimu kwa wanufaika ili waweze kujitegemea katika maisha yao baada ya kukoma kwa ruzuku.

Mkurugenzi ameagiza maafisa biashara wake kujikita katika kutoa elimu kwa wanufaika hao ili waweze kuendesha biashara zao kwa uweledi.

“Kaya maskini katika halmashauri yangu zipo nyingi, kwani katika mchakato wa awamu ya pili zilijitokeza kaya 6000 ambazo zilikuwa zinastahili kupata ruzuku lakini walioingia kwenye mpango ni kaya 1,026 pekee,” amesema Msigala.

Mkugenzi amesema mahitaji ni makubwa hivyo ni vema kwa walionufaika kujikwamua kiuchumi watoke nje ya mpango ili waingie wanufaika wengine.



Mnufaika wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,  awamu ya pili, Rahel Mpanda kutoka kijiji cha Sango, kitongoji cha Kombe kata ya Kimochi, akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokuwa ziarani mkoa wa Kilimanjaro kuangalia Maendeleo ya wanufaika hao baada ya kupokea ruzuku zao.


Mnufaika wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii TASAF,  awamu ya pili, Rahel Mpanda kutoka kijiji cha Sango, kitongoji cha Kombe kata ya Kimochi, akiwa nje ya nyumba yake aliyokuwa akiishi kabla ya kuingizwa kwenye mpango wa Tasaf kwa kupewa ruzuku ilimuwezesha kujenga nyumba ya kudumu.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakizungumza na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Moshi Vijijini mara baada ya kumaliza ziara yao wa kuwatembelea wanufaiaka wa Tasaf wa mkoani Kilimanjaro
Rahel Mpanda akiwa na mifugo yake aliyoipata kutokana na ruzuku ya Tasaf.
Mkurugenzi wa Halmashauri ya ya Moshi Vijijini,  Castory Msigala, akizungumza na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari waliokuwa ziarani mkoani Kilimanjaro kuangalia wanufaika wa mradi wa Tasaf.
Mnufaika wa mfuko wa Maendeleo kwa Jamii( TASAF ) Rahel Mpanda, akiwarudisha bandani Ng'ombe wake aliowanunua kwa Ruzuku ya Tasaf  aliyoipata baada ya kuingizwa kwenye ya Tasaf mpango mara baada ya kuingizwa kwenye mpango wa kaya masikini.



Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...