Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari, wakiwa wameketi nje ya nyumba ya Theresia Masawe aliyoijenga kwa ruzuku ya Tasaf.
Theresia Masawe mkazi wa kijiji cha Kombo kata ya Kibosho, Moshi vijijjni mkoani Kilimanjaro, kushoto mwenye tisheti ya mistari, akiongea na wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari nchini, kujua namna alivyonufaika na Mpango wa Tasaf wa kuinua kaya maskini wakati wa ziara ya wahariri hao mkoani Kilimanjaro hivi karibuni.
Yusta Soka akipelekea mkungu wa ndizi sokoni, yusta ni mmoja wa anufaika wa TASAF ambaye sasa anaendesha maisha yake bila wasiwasi kufuatia ruzuku anayoipata kutoka Tasaf kwa kuzalisha na kumpatia faida.
Mnufaika wa mfuko wa Maendeleo kwa Jamii( TASAF ) Yusta Soka akionyesha Ng'ombe wake aliowanunua kwa Ruzuku ya Tasaf iyoipata baada ya kuingizwa kwenye ya Tasaf mpango mara baada ya kuingizwa kwenye mpango wa kaya masikini.
MTENDAJI wa kata ya Kibosho Magharibi, Wilaya ya Moshi Vijijini Mkoani Kilimanjaro, John Masawe ameishauri Serikali na wadau wa mpango wa Maendeleo ya Jamii kusaidia kaya maskini TASAF kupanua wigo kwa wanufaika kwa kuwapatia msaada mkubwa zaidi ili waweze kuacha kuwa wategenezi.
Masawe ambaye pia ni Mtendaji wa kijiji cha kijiji cha Kombo amesema hayo alipokuwa akiongea na wahariri wa vyombo mbali mbali vya habari waliokuwa ziarani mkoani humo hivi karibuni.
Amesema, mpango wa TASAF ni mzuri na umekuwa na mafanikio mengi na makubwa kwa kaya mbali mbali hivyo kama wakiendelea kusaidiwa kwa kupewa elimu basi kile kidogo wanachotumiwa wanaweza kukifanyia kazi kwa ufasaha ili kuondokana na utegemezi
Amesema, zipo kaya ambazo kile kidogo wanachotumiwa wanakifanyia kazi na kuongeza faida kwa haraka,
"Kuna mtu ukimpa kidogo anaweza kukiambia nacho kwa spidi kubwa hivyo basi ni vema akapatiwa elimu kuendana na spidi yake ili mwisho wa siku aje kutoka kwenye utegemezi" amesema Masawe.
Amesema Kijiji cha Kombo kipo katikati ya Wilaya ya Moshi Vijijini, mkoani Kilimanjaro ni kijiji mojawapo ambacho kinanufaika na mpango wa Tasaf kati ya vijiji 10 vinavyounda Kata ya Kibosho Magharibi.
Amesema, mpango huo wakati unakuja uliingia kwa vijiji sita kati ya saba vilivyokuwepo wakati huo, ambapo kutokana na uhitaji wa jamii vijiji vitatu viligawanyika vikawa vijiji 10, lakini vile vilivyogawanyika wale walengwa waliendelea kupata huduma kutoka kwenye kijiji mama.
Amesema kati ya hivyo vijiji kimoja hakikuwepo kwenye mpango wa TASAF, lakini maelezo ya Serikali ya mwaka 2020 kumekuwepo na taratibu wa kuibua kaya na kwa bahati nzuri vile vijiji mama vimekuwa na mpango mwenyewe.
"Asilimia kubwa katika kijiji changu kaya zinazonufaika ni 54, kuna watoto waliokuwepo kwenye utaratibu wale watoto wa chini ya miaka mitano,wanufaika wengine ni watoto wa shule za msingi na sekondari hadi kidato cha nne huku wale wanaomaliza darasa la saba na kidato cha nne kama hawataendelea na shule wanaondolewa kwenye mpango". Amesema Masawe.
"Mpango huu ni mzuri kuna watu kwa kweli leo hii tungekuwa tunawaita majina mengine, lakini wanaendelea kuwepo kutokana na mpango wa Tasaf,
Kuna watoto kama wasingepata huduma stahiki kama za afya na elimu kupitia mpango wa Tasaf wasingeweza kutimiza malengo yao na pia wapo vikongwe wengine ambao uenda leo wasingekuwepo, lakini msaada wanaoupata kutoka Tasaf wameweza kupata chakula na mambo mengine.
Kwa upande wake, mnufaika wa mpango wa kunusuru Kaya maskini kipindi cha pili awamu ya tatu, Anna Soka anaishukuru sana Tasaf kwani imemuwezesha kwa kiwango kikubwa na kumfanya aondokane na maisha duni aliyokuwa kuishi kwa miaka mingi.
Amesema kabla ya mpango huu kuanza alikuwa akishi maisha ya ya tabu kwenye nyumba ya tope yeye na mwanae huku mlo wake ukitokana na kulima mashamba ya watu na kukatia ngo'ombe za watu majani.
"Naishukuru sana Tasaf, nilianza kwa kupata Sh 30,000 ambazo nilianzisha biashara kidogo ya kununua mikungu 10 ya ndizi na pia nilajiunga kwenye kikundi cha Tasaf huku nikiendelea kuuza ndizi". Amesema Soka.
Amesema, faida aliyokuwa akiipata kutokana na biashara ya Ndizi na kwenye kikundi ilimuwezesha kukopa fedha kwenye kikundi hicho na kununua ndama ambaye baada ya kukua alimuuza kwa Sh 900,000 ambazo alinunua mawe na mchanga teyari kwa kuanza ujenzi.
Amesema kupitia kikundi cha Tasaf aliweza kusimama imara na kujenga nyumba ya matofali hadi kufanikiwa kuweka umeme
Hata hivyo, Soka amesema, pamoja na mafanikio hayo, bado anahitaji sana msaada wa Tasaf ili aendelee kusimama vema na iwapo ikitokea msaada huo utasimama basi yeye anaweza hata kupoteza maisha.
Naye, Teresia Masawe (59), amesema wakati anaingia kwenye mpango huo wa Tassaf mwaka 2014 alianza kwa kwa kulipwa sh. 60,00 ambazo baadae zikapungua hadi 48,000.
Amesema, katika Sh.60,000 alichukua sh. 55,000 akanunua mikungu kumi ya ndizi ambayo aliweza kuzalisha na kupata faida ambapo sasa anauwezo wa kulipia watoto wake ada na kuongeza mtaji hadi kufikia mikungu 30.
"Wakati naingizwa kwenye mpango kwenye kaya yangu tulikuwa watu sita pamoja na wanangu, baadae wawili walitoka na kwenda kujitegemea.
"Nilijiunga na mfuko wa Tasaf mwaka 2014 na mwaka 2015 nilianza kwa kuanza kulipwa Sh. 60,000, ambapo kwa imeshuka hadi Sh 48,000, nilipoanza kupata Sh 60,000 nilikuwa na watoto wawili wa sekondari, mjukuu mmoja alikuwa bado hajaanza shule, nilianza kufanya biashara kwa kununua mikungu ya ndizi na kupeleka Moshi mjini.
Katika hiyo hela, alichukua sh 55,000 akanunua mikungu ya ndizi kwa mara ya kwanza na Sh 5,000 alinunua chakula nyumbani, niliendelea kupata faida ikanisaidia kwa watoto shule na kuongeza idadi ya mikungu kutoka 10 hadi 30
"Niliendelea kupata faida, nikajiunga kwenye kikundi cha kikoba na pia nikajiunga na kikundi cha wakina mama wa mpango wa Tasaf, kwa hiyo watoto waliendelea vizuri shuleni kutokana na faida niliyokuwa napata,"
Amesema kwenye kikoba alikopa sh 300,000 akanunua nguruwe wanne, baadae akawauza akapa Sh milioni moja na laki mbili, akanunua Ng'ombe mmoja akazaa dume ambaye badae alimuuza Sh 500,000 akanunua Nguruwe wanne.
Massawe anaishukuru sana Tasaf kwa kubadirisha maisha yake kwani kabla ya hapo nilikuwa na maisha magumu yasiyokuwa ya uhakika, lakini sasa anafurahia maisha yake, kwani kutoka na Tasaf pia ameweza kujenga nyumba imara ya kuishi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...