Katika kuadhimisha siku ya Kimataifa ya Usafiri wa Anga Duniani (ICAD), Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) imetoa msaada wa vitanda (double decker) 26 kwa Shule ya Sekondari Azania iliyopo Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya kurudisha kwa jamii (Corporate Social Responsibility).
Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo, Kaimu Mkurugenzi wa Jiji Dar es Salaam, Bi. Tabu Shaibu amesema kwamba TCAA imefanya jambo la muhimu la kuunga mkono juhudi za Serikali katika masuala ya elimu nchini.
"TCAA mmekuwa ni mdau muhimu sana na tunawashukuru kwa kutoa msaada wa double decker 26 zinazoenda kusaidia wanafunzi 52", ameeleza Bi. Tabu.
Akizungumza kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu TCAA, Meneja Ununuzi wa Mamlaka hiyo Bw. Yoswan Nyongera amesema kuwa "sisi kama TCAA tumefurahi sana kufanikisha hili kwa kuwa tunatambua umuhimu wa elimu kwa watoto wetu. Tunajua mahitaji ni mengi lakini kwa hiki kidogo kitaenda kupunguza changamoto ya vitanda kwa vijana wetu".
Naye Mkuu wa shule ya Sekondari ya Azania Bw.Melisius S. Kayombo ameeleza kuwa, " TCAA mmefanya jambo kubwa sana kwetu na niwaahidi kwamba, matokeo ya hiki mlichokifanya mtakuja kuyaona. Tunawaahidi kuwa watoto wetu wanaenda kuwa na ufaulu wa hali ya juu kwa kuwa wanaenda pata utulivu".
Akizungumza kwa niaba ya Afisa Elimu Sekondari wa Jiji la Dar es Salaam, Dkt. Wema Chamshama ameeleza kuwa TCAA imeweka alama kubwa Azania Sekondari na kwenye Sekta ya elimu na ameiomba Mamlaka hiyo kuendelea kutoa mchango wake kwenye maeneo mengine ikiwemo madawati na matundu ya vyoo.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikata utepe kuashiria uzinduzi wa makabidhiano ya vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam. Wa pili kulia ni Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikagua vitanda vilivyotolewa na Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Desemba 06, 2021. Kulia ni Meneja Ununuzi wa TCAA Bw. Yoswan Nyongera aliyemwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo
Mkuu wa Shule ya Sekondari Azania Bw. Melisius D. Kayombo(wa pili kulia) akitoa maelezo kuhusu vitanda kwa mgeni rasmi Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Tabu Shaibu mara baada ya kupokea vitanda hivyo kutoka TCAA leo Desemba 06, 2021. Kulia ni Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akielezea namna Serikali inavyotambua mchango wa TCAA kwa jamii mara baada ya Mamlaka hiyo kukabidi vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam.
Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu akikabidhi Cheti kwa Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera kwa niaba ya Mamlaka hiyo kwa kujitoa kusaidia jamii hasa kwenye Shule mbalimbali hapa nchini.
Meneja Ununuzi wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA) Yoswan Nyongera akizungumza kuhusu namna Mamlaka hiyo ilivyojipanga kuendelea kurudisha kwa jamii hasa kwenye Shule mbalimbali za hapa nchini mara baada ya kukabidhi vitanda (double decker) 26 katika Shule ya Sekondari Azania iliyopo jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya vitanda vilivyokabidhiwa shule ya Sekondari Azania kutoka kwa Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
Meneja Mawasiliano na Uhusiano TCAA Bi. Salome Mallamia akitoa utambulisho kwa Kaimu Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam Bi. Tabu Shaibu mara baada ya kuwasili katika Shule ya Sekondari Azania wakati wa kukabidhi msaada wa vitanda (double decker) 26 katika Shule hiyo
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...