KATIKA kuelekea Maadhimisho ya Miaka 60 ya Uhuru, Wanachuo kutoka Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) wamevunja rekodi ya kupanda Mlima kilimanjaro kwa siku 3 tu badala ya siku 6 kama ambavyo imezoeleka kwa watu wengine wanaopanda mlima huo.
Wanachuo hao wa Taasisi ya Uhasibu Tanzania Innocent George Masanja anayesoma Shahada ya Uongozi wa Rasilimali watu na Fadhili Jonathan Naaman anayesoma Shahada ya Usimamizi wa Biashara wamepanda Mlima Kilimanjaro mapema wiki hii.
Tukio hili la kihistoria limeipeperusha bendera ya Taasisi ya Uhasibu (TIA) kitaifa na kimataifa, na hakika TIA inajivunia kuwa na vijana Shupavu, Jasiri na wachapakazi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...