Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Mhe. Stephen Kagaigai amehitimisha zoezi la kupanda Mlima Kilimanjaro kwa ajili ya maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru. Hitimisho hilo limeenda sambamba na kuwapokea watu mbalimbali waliopanda Mlima Kilimanjaro wakiongozwa na aliyeshika bendera Kanali Martin Msumali na Staff Surgent Samwel Chacha ambao walienda kusimika bendera ya Tanzania kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro tarehe 10 Disemba, 2021.
Meneja wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi Riganda ameiwakilisha vyema TIC kwa kuweza kupanda na kufika kilele cha Mlima Kilimanjaro.
Bw. Riganda amekuwa kati ya watu 79 waliofanikiwa kufikia kilele cha Mlima Kilimanjaro ambapo waliopanda awali walikuwa 150.
Riganda amesema kuwa safari ya kupanda mlima Kilimanjaro ilianza tarehe 5 Desemba, 2021 kutokea Geti la Marangu hadi kambi ya Mandara ambapo ilichukua masaa 4 kwa kusafiri urefu kwa futi 8,858.
Siku
ya pili safari ilianza Mandara hadi kambi ya Horombo kwa kusafiri urefu
wa futi 12,205 ambayo ilichukua masaa 6. Siku ya tatu safari ilianza
Horombo hadi Mawenzi ridges kwa kusafiri urefu wa futi 14,400 kwa ajili
ya kuzoea mazingira ya hewa (climatization) kabla ya kupanda zaidi mlima
kuelekea Kibo.
Siku
ya nne safari ilianza Horombo hadi kambi ya Kibo kwa kusafiri urefu wa
futi 15,530 safari ambayo ilichukua masaa 6. Siku ya tano safari ilianza
Kibo Hut hadi kilele cha Mlima Kilimanjaro (Uhuru Peak) kupitia
Gilman's Peak na Stella Peak kwa kusafiri urefu wa futi 19,341
ambayoilichukua masaa 10. Siku ya sita safari ilianza kurudi Geti la
Marangu.
Bw. Riganda amesema kuwa alienda na kauli mbiu ya WEKEZA TANZANIA ARDHI YENYE MLIMA KILIMANJARO (INVEST IN TANZANIA THE LAND OF MOUNT KILIMANJARO).
Bw. Riganda amesema kuwa amefurahia sana safari hiyo kwani ameweza kukutana na baadhi ya vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje kama vile BBC (Salum Kikeke), ITV, TBC, na wengine waliokuwa katika ziara hiyo. Vilevile amefanya mahojiano na balozi wa hiyari wa utalii kutoka Marekani Mr. Macon Dunnagan ambae amemweleza fursa za uwekezaji tulizonazo Tanzania na akaahidi kuwa atazitangaza hizo fursa hizo. Mr. Dunnagan amepanda Mlima Kilimanjaro zaidi ya mara arobaini na tano (45)
Hafla hiyo imehudhuliwa na Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro Bw. Stephen Kagaigai, Mwenyekiti wa Bodi wa TANAPA Jenerali George Waitara, Katibu Tawala wa Wilaya ya Moshi Bi. Angelina Marko na Viongozi mbalimbali wa Serikali, Sekta binafsi na Makampuni mbalimbali ya utalii.

Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi
Riganda akiwa kwenye kilele cha Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha
miaka 60 ya Uhuru tarehe 9 Disemba, 2021.

Riganda akiwa kwenye eneo la Kibo alipokuwa akipanda Mlima Kilimanjaro
katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 6 Disemba, 2021.
Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi
Riganda akiwa njiani kuelekea kilele cha Mlima Kilimanjaro katika
kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 7 Disemba, 2021.
Meneja
wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) Kanda ya Kaskazini Bw. Daudi
Riganda alipokuwa akianza kupanda Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha
miaka 60 ya Uhuru tarehe 5 Disemba, 2021.
Mkuu
wa Mkoa wa Kilimanjaro Stephen Kagaigai akiwapokea waliokuwa wamepanda
Mlima Kilimanjaro katika kuadhimisha miaka 60 ya Uhuru tarehe 10
Disemba, 2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...