Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Afya) Dkt. Grace Magembe amewataka wataalam wa afya na wadau kushirikiana kutoa elimu juu ya ugonjwa wa Selimundu(Sickle Cell).

Dkt.Grace amesema hayo Desemba 7, 2021 Jijini Dodoma wakati akipokea ripoti ya Tanzania Sickle Cell Disease Alliance (TANSCDA) iliyoeleza jinsi ilivyotoa elimu ya upimaji na jinsi ya kujikinga juu ya ugonjwa wa selimundu katika mashule na vyuo Tanzania.

Amesema pamoja na takwimu kuonesha Tanzania jumla ya watoto 11,000 kila mwaka wanazaliwa na ugonjwa wa selimundu na kwa upande wa Mikoa ya Kanda ya Ziwa na Pwani tatizo ni kubwa, amewataka wataalam wa afya kuhakikisha kunakuwepo na mashine zitakazo tambua mgonjwa mwenye vinasaba vya selimundu(Sickle Cell) mapema ili kusaidia kupata matibabu kwa haraka.

“kwenye masuala ya kuangalia afya ya jamii hatuangalii gharama ndio mana kuna gharama Serikali hua inazibeba sababu suala hili linagusa afya ya kila mtanzania” amesema Dkt. Grace

Ametoa wito kwa jamii kuto wanyanyapaa wagonjwa wa selimundu na kuwataka wataalam na wadau kutumia njia rahisi ya mawasiliano ambayo itatoa ujumbe na elimu kwa jamii juu ya ungonjwa wa selimundu.

“Ni vizuri pia kuwapatia elimu viongozi wetu wa dini na kimila wa kijua elimu kuhusu ugonjwa wa selimundu ni vizuri itasaidia wao kutoa sababu asilimia kubwa ndoa zinafungwa kanisani na msikitini wakijua hii elimu watatusaidia kuitoa kwa jamii” amesisitiza Dkt. Grace

Mtendaji Mkuu, Tanzania Sickle Cell Disease Alliance (TANSCDA) Dkt. Deogratias Soka ameishukuru Serikali na kuiomba kuendelea kuiunga mkono taasisi hiyo ili kuendelea kutoa elimu kwa jamii.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...