Na Said Mwishehe, Michuzi TV

VIONGOZI wa Taasisi ya Kilimo Hai Tanzania (TOAM) wamesema kuna kila sababu Serikali kwa kushirikiana na wadau wa kilimo nchini kuhakisha kunakuwa na sera na miongozo itakayosimamia uzalishaji chakula ambao utakuwa salama.

Wamesema hayo jijini Dar es Salaam wakati wakizungumza na waandishi wa habari kuhusu matokeo ya utafiti yaliyofanywa na Taasisi ya The Alliance for Food Sovereignty in Africa (AFSA), kwa lengo la kuangalia sera ya uzalishaji chakula Afrika, ambapo matokeo hayo yameonesha kwa sera zilizopo zinakinzana , hivyo kusababisha kukosekana kwa sera na miongozo itakayosimamia uzalishaji chakula ulio salama.

Mtendaji Mkuu wa TOAM, Bakari Mongo amefafanua taasisi hiyo ilianzishwa Juni 2015 na majukumu yake ni kuratibu maendeleo ya kilimo hai nchini na inafanya kazi kupitia mradi ya ufadhili.

Pia ni taasisi inayotoa huduma maeneo yote nchini lakini kuna maeneo yameanishwa kulingana na majitaji ya mradi.

"Sasa tumewaiteni kwasababu ya suala 

moja tu  la kuangalia ni namna gani mifumo ya uzalishaji Tanzania na duniani kwa ujumla imekuwa ikiendelea lakini naweza kusema uzalishaji wa chakula kokote duniani unaathiriwa na vigezo vingi.Kigezo kimoja wapo ni sera zinazohusiana na uzalihaji, kuna sera ya kilimo, sera mazingira na pia shughuli za wanadamu ambazo zinachangia kwa sehemu kubwa uzalishaji kuwa mzuri au mbaya na usio salama.

"Tuna viumbe hai na baianoai mbalimbali kwa jumla ambavyo vinazunguka mazingira ya uzalishaji, maana uzalishaji unahitaji viumbe hai vya akila aina, lakini tuna mifmo ambayo sio mifumo ya nchi yetu peke yake, kuna mifumo ya kidunia, kuna mifumo ya kibiashara , hii pia inachangia kuathiri.

"Kwa mfano pembejeo za kilimo ambazo tunazitumia hapa nchini , sio zote tunazalisha sisi, maana yake zinatoka nje ya nchi na hiyo ni biashara , kama ni biashara kila anayeifanya anajitahidi kukuwa na kupata faida au tija inayostahili.

Kwa kifupi kupitia wenzetu wa Afrika Food Alliance tumefanya utafiti kuangalia namna gani sera na  miongozo ya Serikali inayoweza kusaidia katika uzalishaji salama wa chakula au uzalishaji usio salama,"amesema Mongo.

Ameongeza katika utafiti huo kilichooekana kuna changamoto nyingi zinazoukumbuka huo mfumo huku akisisitiza kuna masuala ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yamekuwa ni wimbo wa duniani kote,wanashuhudia  athari za mabadiliko ya tabianchi ikiwemo uwepo wa joto kubwa, mvua hazinyeshi kwa wakati kama walivyozoea na hazinyeshi kwa mgawanyo wake.

"Kuna uharibu mkubwa wa mazingira unaonekana wazi na unachangia kwa sehemu kubwa kuathiri uzalishaji wa mazao ya kila aina yakiwemo mazao ya mifugo,mimea na hata samaki kwani ukiharibu maji samaki uzalishaji unakuwa sio mzuri.Kuna mazingira ya kisera yasiyo rafiki yanayochangia upungufu wa chakula. Kumbuka hatusemi upungufu wa chakula tu lakini ni chakula ambacho ni salama kwa mlaji,'amesema.

Ameeleza kwa hiyo kama sera zilizopo hazitoi muongozo katika kutumia pembejeo na mbegu ambazo ni salama kwa mjali bado kunakuwa na tatizo.Unaweza kukutana kuna sera ya kuhimiza matumizi ya mbolea za viwandani ambazo hazitoe mianya ya kutumia pembejeo mbadala kama mboji na samadi.

"Na sio kwenye kuzalisha tu hata kwenye uhifadhi , kuna maneo mengine unakuta watu wanatumia dawa ya kuua viwavijeshi ili mahindi yakae muda mrefu.Kwa kifupi tukiangalia mifumo ya uzalishaji chakula salama ,tuzalishe chakula cha kutosha lakini ambacho kitakuwa salama, tunahitaji sera zetu zishabiihane na sio zisikinzane, hilo ni jambo la msingi sana.

"Pia tunahitaji elimu ya kutosha kwa wakulima wetu na watalaamu wetu waweze kutumia mbinu sahihi , sasa hivi tunaishukuru Serikali kwasababu ya usikivu na kukubaliana na sisi kwa kutengeneza mkakati wa kilimo hai na tumeanza mchakato kwa maelekzo ya Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo , ambapo tunategemea ukienda vizuri Agosti mwakani utazinduliwa.

Kwa kifupi baadhi ya sera kikunzana bado ni tatizo lakini sio tu kukinza, sera bado hazitoi njia mbadala zitakazomsaidia mkulima kuzalisha chakula cha kutosha na salama".

Kwa upande wake Mshawishaji wa Kilimo Hai,  Paul Chilewa amesema mfumo wa uzalishaji chakula uliopo sasa unawatoa wengi ndani , akitoa mfano Tanzania na Afrika wanategemea wazalishaj wadogo lakini ukiangalia sera na mfumo mzima wa chakula hautoi msaada wa kuhakikisha wakulima wadogo wanaendelea kuzalisha kwa maana ya kupata mbegu , masomo na vitu vingine.

"Hilo ni tatizo la kwanza, kwa hiyo tunaposema sera zote tunataka zihakikishe ushirikishwaji, mfumo uhakikishe wale wazalishaji wadogo wanapata mahitaji yao.

Mifumo iliyopewa kipaumbele wakati mwingine inaharibu mazingira, kwa hiyo tunasema sera zihakikishe watu wanashiriki kuzalisha na kukipata chakula,'amesema.

Wakati huo huo Abdllah Ramadhan ambaye ni Mratibu wa Shirika lisilo la Kiserikali linalojishughulisha na Utunzaji wa Bioanuai Tanzania (TABIO), ameongeza wanapozungumzia sera ziwe rafiki katika kuhakikisha kunakuwa na  mfumo wa uzalishaji chakula ambao ni endelevu na salama.

"Tuwe na sera ambazo zinashabiihiana na sio zinazokinzana,kwa hiyo utafiti uliofanyika umeangalia ni namna gani tutakuwa na sera ya Afrika ya uzalishaji chakula.

"Kwa Afrika nzima hakuna hiyo sera na hata ukija kwa ngazi ya taifa, tuna sera ya chakula na lishe ya mwaka 2002, ukiisoma ile sera utakuta haijaweza kubeba hii dhana ya mfumo wa uzalishaji chakula kwa mapana yake , sera kama ile inaweza kufanyiwa maboresho ikabeba hii dhana ya mfumo wa chakula lakini bado mle ndani kuna mapungufu, kwa hiyo kwa Tanzania sera ile inaweza kufanyiwa maboresho au kukawa na sera inayojitegemea.

"Kwa hiyo tunatakiwa  tuwe na sera inayobeba masuala mtambuka kwa mapana yake ili tuje na mfumo unaoeweleka, maana hili ni tatizo , zamani kama mnakumbuka mkisia magonjwa kama sukari au presha yalikuwa ni magonjwa ya wenye uwezo lakini sasa hivi haijalishi, umri, uwezo , unapesa au huna yanamkumbuka kila mtu katika jamii.

"Pamoja na kuwa makini katika ulaji, je tunachokuwa kiko salama?Kwa hiyo haya lazima tuyazungumze kwa mapana yake ili Serikal iyafanyie kazi, hata katika kipindi hiki ambacho Serkali inahamasisha kuongeza uzalishaji , lakini chakula kiwe salama.Tukipigie debe kilimo hai maana mbinu za kilimo hai zinatuwezesha kuzalisha chakula cha kutosha na salama."

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Kilomo Hai Tanzania(TOAM) Bakari Mongo( wa kwanza kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu umuhimu wa kuwa na sera na miongozo kwa ajili ya kusimamia uzalishaji chakula ulio salama .
Mshawishi wa Kilimo Hai Paul Chilewa(katikati) akisisitiza jambo mbele ya waandishi wa habari.Kushoto ni Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Utunzaji wa Bioanuai Tanzania(TABIO) Abdallah Ramadhan na kulia ni Mtendaji Mkuu wa TOAM Bakari Mongo
Mtendaji Mkuu wa TOAM Bakari Mongo akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa Watanzania na Waafrika kujikita katika Kilimo hai
Paul Chilewe ambaye ni Mshawishi wa Kilimo Hai akitoa mifano kadhaa inayoonesha kutokuwa na mifumo inayowezesha wakulima wadogowadogo kushiriki kikamilifu katika kuzalisha chakula salama

Mratibu wa Shirika lisilo la kiserikali linaloshughulikia Utunzaji wa Bioanuai Tanzania( TABIO) Abdallah Ramadhan (katikati) akisisitiza jambo .

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...