Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Usambazaji, Maduka na Huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, George Lugata akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)wakati wa uzinduzi wa huduma ya manunuzi ya simu janja kwa mkopo ambayo Vodacom Tanzania PLC kwa kushirikiana na D. Light inaleta wateja wake.huduma hiyo umelenga kutatua changamoto kubwa inayorudisha nyuma matumizi ya simu janja.

Lugata ametoa wito kwa wateja wote wa Vodacom kuchangamkia fursa katika msimu huu wa sikukuu kuhakikisha wanachangamkia fursa ya kupata au kumnunulia umpendaye simujanja ili afaidike na ulimwengu wa kidijitali leo jiji jijini Dar es Salaam
Mkuu wa kitengo cha Mauzo, Usambazaji, Maduka na Huduma kwa wateja Vodacom Tanzania PLC, George Lugata(kulia) akielezea namna unavyoweza kulipia simu hiyo mteja wa Vodacom atakiwa kulipia Tsh 80,000 tu na ataondoka na simu yake, halafu atakuwa akilipia shilingi 1,800 kwa siku kwa muda wa siku 300 ili kumaliza deni analodaiwa leo jijini Dar es Salaam.kushoto ni Mkurugenzi wa D.Light Tanzania , Charles Natai.

Mkurugenzi wa D.Light Tanzania,Charles Natai akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) juu lengo kuu la kuwapa Watanzania wengi zaidi fursa ya kumiliki simujanja ili waweze kufaidika na huduma mbalimbali zinazopatikana kupitia mfumo wa kidijitali leo jijini Dar es Salaam.(kulia)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...