Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi. Robert Gabriel (katikati) akikata
utepe wakati wa ufunguzi wa duka la kisasa la kampuni ya Vodacom jijini
Mwanza, duka hilo linaongeza idadi ya maduka ya kampuni hiyo yaliopo
jijini humo kwa kuwarahisishia wateja wake kupata huduma kwa ukaribu
hasa kipindi hiki cha sikukuu kwa ku "Show Love" kwa wapendanao kupitia
promosheni ya "Tule Shangwe" na wateja kujishindia zawadi mbalimbali.
Wengine ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda Riwa
{wapili kulia}, Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya
(kulia), na Mkuu wa wilaya ya Ilemela, Hassan Masala (mwenye tai).
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza, Mhandisi. Robert Gabriel (kushoto) akikata keki
wakati wa ufunguzi wa duka la kisasa la kampuni ya Vodacom jijini
Mwanza, Katikati ni Mkurugenzi wa Biashara Vodacom Tanzania PLC, Linda
Riwa na Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu Kalufya.
Meneja
wa duka la Vodacom tawi la kanda ya Ziwa, Jumeo Iddi (kushoto)
akizungumza na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhandisi Robert Gabriel
(kushoto),wakati wa ufunguzi wa duka la kisasa la Vodacom jijini Mwanza,
na wapili kushoto ni Mkuu wa Mauzo Vodacom kanda ya Ziwa, Ayubu
Kalufya.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...