Na Khadija Kalili
Wakaazi wa Jiji la Dar es Salaam jana usiku walikonga nyoyo zao kwenye tamasha muziki wa Injili 'Christmas Carols 2021' lililorindima kwenye viwanja vya wazi vya Mlimani City Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Ofisa Masoko wa Coca Cola Tanzania Kabula Nshimo alisema kuwa wao ndiyo wadhamini wa tamasha hilo ambalo limefanyika kwa kushirikiana na Kampuni ya Clouds Media Group (MMG) ikiwa ni mahsusi kwa ajili sikuukuu ya Christmas.
Mbali ya wasanii mbalimbali kulitikisa jukwaa na kusisi Mua kwa nyimbo zao mbalimbali pia Nshimo alipanda jukwaani na kuuzindua mtu wa Christmas wa Coke uliitengenezwa kwa ustadi tofauti na tulivyozoea kuona ambao ni ruhusa Kwa wakaazi wa Jini kwenda kupiga picha.
Tamasha hilo ambalo lilifunguliwa na Mtangazaji nguli Harris Kapiga, lilipambwa na waimbaji waliofanya makubwa ambao ni Mimi Mars, Paul Clement, Joel Lwaga, Good luck Gozbert.
Wengine ni Parform Irene Robert, Ikupa Mwambenja, Derrick Marton, Beda Adrew, Maggie Muliri, Atosha Kissava, Christmas Carols na MC Madevu, Bwagamoyo to Jesus.
Wengine walioimba na kumtukuza Mungu ni RC Kigamboni, Borne Kings, Ushindi Kwaya kutoka Ufunuo Buza, Baragumu Kwaya Deakonias.
Waimbaji wengine ni Neema Gospel Ambwene Mwasongwe, Barnaba Classic, Essence of worship, Rose Muhando, KKKT Kijitonyama.
Tamasha la mwaka huu wa 2021unatajwa kuwa wa tofauti na Clouds kutokana na kulifanya Kwa ajili ya kumshukuru Mungu kuwavusha katika mambo mengi.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...