Wajasiriamali kutoka nchi ya Burundi wakionesha bidhaa zao kwa washiriki wa maonesho ya 21 ya wajasiriamali ya Afrika Mashariki(EAC) maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi" yanayoendelea eneo la Rock City jijini Mwanza,wajasiriamali kutoka nchi sita wanaonesha na kuuza bidhaa zao.
Wananchi waliotembelea maonesho ya 21 ya wajasiriamali nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) yanayojulikana maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi" yanayoendelea eneo la Rock City jijini Mwanza.
Wananchi waliotembelea maonesho ya 21 ya wajasiriamali kwenye nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki(EAC) maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi" wakiangalia bidhaa mbalimbali zinazouzwa na wajasiriamali hao eneo la Rock City jijini Mwanza.
Mmoja wa wajasiriamali kutoka jijini Arusha akipanga bidhaa zake wakati akisubiri wateja wake eneo la Rock City jijini Mwanza ambako kunaendelea maonesho ya wajasiriamali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi".
Wajasiriamali kutoka nchi sita wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wakionesha bidhaa zao kwa washiriki wa maonesho ya 21 ya wajasiriamali ya "Jua Kali,Nguvu Kazi" yanayoendelea eneo la Rock City jijini Mwanza.
Mmoja wa wajasiriamali kutoka mjini Moshi akionesha viatu vilivyotengezwa hapa nchini eneo la Rock City jijini Mwanza ambako kunaendelea maonesho ya wajasiriamali ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi".
Wajasiriamali kutoka nchini Burundi wakionesha bidhaa zao kwa washiriki wa maonesho ya 21 ya wajasiriamali ya Afrika Mashariki(EAC) maarufu "Jua Kali,Nguvu Kazi" yanayoendelea eneo la Rock City jijini Mwanza.
Burudani ya utamaduni kutoka nchini Rwanda imekua kivutio kwa washiriki wa maonesho hayo yanayotarajiwa kufungwa Desemba 12,2021.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...