Na Mwandishi Wetu,Mvomero
WAKALA wa Huduma za Misitu(TFS) umemkabidhi mizinga ya nyuki katika Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro kwa lengo la kuhamasisha ufugaji nyuki endelevu.
Mizinga hiyo imekabidhiwa kwa Mkurugenzi Wa Wilaya ya Mvomero mkoani Morogoro aliyepokea kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo Halima Okash
Akizungumza wakati wa kukabidhi mizinga hiyo Desemba 6,2021 katika ofisi ya Kituo Cha Msitu wa mazingira asilia Mkingu, Kamanda Msaidizi Rasilimali za Misitu kutoka TFS Bernadetha Kadala amesema lengo na dhumuni la ugawaji wa mizinga hiyo ni kutia chachu na kuchochea ufugaji endelevu wa nyuki katika Msitu wa mazingira Asilia Mkingu.
Aidha Kadala amesema thamani ya mizinga hiyo 85 ni Sh.10,200,000 na itagawiwa kwa vikundi sita vya ufugaji nyuki vinavyofanya shughuli zao za ufugaji nyuki kuzunguka hifadhi ili kuleta chachu na kuchochea kilimo cha ufuguji nyuki katika Hifadhi Ya msitu Asilia Mkingu.
Hifadhi ya msitu wa mazingira Asilia Mkingu iliyo chini ya Wakala Wa Huduma za Misitu Tanzania ni miongoni nwa hifadhi 20 za misitu ya serikali kuu zilizopandishwa hadhi ya uhifadhi kuwa Hifadhi za mazingira nchini.Hifadhi hiyo inazungukwa na vijiji 25, vyenye idadi ya wakazi wapatao 61,000 wanaojishughulisha na uzalishaji mali ikiwemo kilimo na ufuguji.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya Mvomero Hassan Njama Hassan ametoa shukrani kwa TFS kwa kuona umuhimu wa kutoa mizinga hiyo ambayo inakwenda kubadilisha ufugaji nyuki kutoka ule wa mazoea na kuwa wa kisasa, na kwamba mizinga hiyo italindwa na kutunzwa ili kuleta tija.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...