Na Mwandishi wetu – Arusha
Wakulima katika skimu za kilimo cha umwagiliaji Mkoani Arusha, wamepewa elimu kuhusiana na namna ya kusajili vyama vya umwagiliaji na utoaji wa ada na tozo na kupewa utaratibu wa kulipia ada hizo zitakazosaidia kuboresha na kurekebisha miundombinu ya kilimo cha umwagiliaji pale itakapokumbwa na madhara yatokananyo na athari za mabadiliko ya tabianchi au uchakavu.
Bi Fatuma Mwera Afisa Kilimo kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji akizungumza na baadhi ya viongozi wa skimu za kilimo cha umwagiliaji katika Halmashauri ya Arusha katika kata ya Ilikiding’a alibainisha kuwa, usajili wa vyama vya umwagiliaji utasaidia skimu kutambulika na kupata fursa zinazojitokeza ikiwa ni pamoja na kupelekewa miradi ya ujenzi wa miundombinu ya umwagiliaji.
Aidha aliwaasa viongozi hao kuwa vinara katika swala zima la usimamizi na utunzaji wa mazingira hususan vyanzo vya maji ikiwa ni pamoja na kutokufanya shughuli za kibinadamu katika vyanzo hivyo.
Aliendelea kusema kuwa, skimu zote za kilimo cha umwagiliaji zitafanyiwa maboresho kwa awamu lakini , skimu ambazo zimesajiliwa ndizo zitakazopewa kipaombele kwanza wakati wa maboresho hayo. “ Ni vizuri kusajili wote kwa pamoja ili tupange mipango ya kazi kirahisi na kuzifikia skimu kwa awamu, Alisisitiza.”
Wataalam kutoka Tume ya Taifa ya Umwagiliaji katika kikao cha pamoja na Afisa Kilimo Umwagiliaji na Ushirika wa Wilaya ya Arusha,hayupo pichani wakijadili kwa pamoja maswala ya tozo za Umwagiliaji.


Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...