Na Amiri Kilagalila, Njombe

INADAIWA kuwa wajawazito katika kijiji cha Makoga wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe,hulazimika kuwakodi wanaume kutoka katika vijiji jirani ili kuwasindikiza kliniki na kuwalipa fedha kutokana na waume zao kugoma kuwasindikiza wake zao kwa kuhofia kupima maambukizi ya VVU.

Wanawake wa kijiji hicho wamebainisha hayo katika maadhimisho ya siku ya Ukimwi kiwilaya yaliyofanyika katika kijiji hicho na kudai kuwa hatua hiyo imetokana pia na waume zao kuwa na ndoa wanawake wengi hali inayowapa uoga kuongozana nao kituo cha afya kwa kuhofia vipimo.


Kufuatia changamoto hiyo wananchi wa kijiji hicho akiwemo Visia Chapile na Athelimo Mwinuka ambaye ni MVIU wakaamua kupaza sauti katika siku ya ukimwi ili kupata msaada wa serikali wa kuwatia nguvuni wanaume wote wanaotelekeza wake zao kipindi cha mimba na kwenda kuishi na wanawake wengine wakihofia kwenda kupima kliniki magonjwa ya kuambukizwa ukiwemo ukimwi kwakuwa kufanya hivyo kunafifisha jitihada za serikali ya kufika sifuri tatu.

“Wanaume wanakataa,naenda kumkodi boda boda ili niweze kupata huduma za afya,nipate kupokelewa na mganga,namchukua boda boda namlipa hela yake naenda kupima kama yule ndio mume wangu wakati sio mume wangu kwa hiyo tunadhalilishana”alisema Visia Chapile

Athelimo Mwinuka amesema “Siku za ujauzito ndio tunapofanikishaga watu wengine kupimwa lakini wengine hawapendi kabisa ndio maana inafika mahali wanakimbia”

Kilio cha akina mama wa kijiji cha Makoga na maeneo jirani ya kata ya Makoga kinathibitishwa na mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Makoga Dr Peter Tamata ambaye anasema akina baba wengi wa kijiji hicho wamekuwa na mitara jambo ambalo anadhani limekuwa likiwapa hofu kwenda na wake zao kliniki kupima afya kipindi cha ujauzito
“Wanaume wengi wanakimbia pindi wanapo mpa mama ujauzito,nah ii hupelekea akina mama kwenda kuchukua wanaume wengine kusimama badala ya yule mhusika aliyempa mimba”alisema Dr Peter Tamata -Mganga Mfawidhi wa kituo cha afya cha Makoga

Kwa upande wake Kaimu Mratibu wa ukimwi wilaya ya Wanging’ombe Atu Fute na Ajira Ngole ambaye ni muuguzi mkuu wilaya Wanging'ombe wakaeleza umuhimu wa kupima na kuanza kutumia dawa na kisha kuhumiza faida ya kupata chanjo ya corona kwa mtu anayeishi na maambukizi ya VVU na magonjwa mengine sugu.

“Wewe uliyeko kwenye dawa kwanza uhakikishe umepima na uwe mfuasi mzuri wa dawa na pia ubaki kwenye dawa vile vile uwe mtoaji wa elimu kwa mwingine ambaye hajawa tayari kupima”alisema Kaimu Mratibu wa ukimwi halmashauri ya Wanging'ombe  ATU FUTE

Wakati maadhimisho hayo yakifanyika kiwilaya katika kijiji hicho,mkoa wa Njombe unaadhimisha katika wilaya ya Ludewa huku kitaifa yakifanyika mkoani Mbeya, na kauli mbiu isemayo "Zingatia usawa tokomeza ukimwi ,Tokomeza magonjwa ya mlipuko".

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...