Mnufaika wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF), Antusa Uchau, akiwa amebeba mkungu wa ndizi teyari kwa kuupeleka Sokoni kuuza ili aweze kupata kipato cha kuendesha maisha yake kufuatia fedha walizopewa na Tasaf.

Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza Mtendaji wa kijiji cha Okaseni kata ya Uru Kusini wakati wa Ziara yao ya kuwatembelea wanufaika wa mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF), mpango wa tatu awamu ya pili mkoani Kilimanjaro.
Mnufaika wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF), Lioba Mushi, akiwa katika eneo la makazi yake kata ya Uru Kusini kijiji cha Okaseni mkoani Kilimanjaro.
Baadhi ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari wakiwa nje ya nyumba ya mnufaika wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya jamii (TASAF), Antusa Uchau, wakati wa ziara yao Mkoani Kilimanjaro. Antusa anajenga nyumba hiyo kufuatia mgao wa sh. 52,000 alizopewa na kuzizalisha kwa kupata faida.
Mtendaji kata, Uru Kusini kijiji cha Okaseni mkoani Kilimanjaro Severin Mende  akizungumza na wahari wa vyombo mbalimbali vya habari wakati wa ziara yao mkoani humo kuwatembelea wanufaika wa mfuko wa  Maendeleo ya Jamii ( TASAF.)


MNUFAIKA wa mpango wa tatu wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF), wa awamu ya kwanza Antusa Uchau (38), ameiomba Serikali kupitia TASAF iwasaidie kuwapatia mitaji zaidi na msingi wa biashara ili waweze kuja kujisimamia zaidi kuendesha maisha yao badala ya kumtegemea pesa peke yake wanazopewa.

Amesema, TASAF imekuwa msaada mkubwa kwa kaya nyingi nchini na kuwafanya waweze kuondokana na shida za chakula na elimu na wakazi.

Antusa ambaye ni mnufaika wa kwanza wa TASAF toka mwaka 2015 ameyasema hayo wakati wa ziara ya wahariri wa vyombo mbalimbali vya habari katika Kata ya Uru Kusini Kitongoji cha Okaseni Kati Kijiji Okaseni Mkoani Kilimanjaro.

Amesema, iwapo TASAF itawapatia msingi yaani mitaji kama vile mabanda ya Nguruwe ama Kuku wanaweza kuendesha biashara zao kwa kuendesha maisha yao kwa urahisi zaidi.  

Antusa amesema, wakati anaingia TASAF alianza kupokea Shilingi 52,000 ambazo alizigawa katika mafungu manne ya  20,000 ambazo alizitumia kwa kununua vifaranga 15 vya kuku na kiasi kingine alikitumia kwa matumizi ya shule ya watoto wake huku pia akianzisha biashara ya ndizi na kijikimu kwa chakula. 

Biashara ya ndizi ilimuwezesha kupata faida ambayo ilimuingiza kwenye vikoba alipokuwa akicheza mchezo wa sh. Elfu tano kwa siku ambao ilipofika muda wa kupokea alipata sh. 400,000 hivyo kukuza mtaji wa ndizi na kuweza kucheza mchezo kwa kiwango cha 10,000.

Amesema, aligajikuwa kuuza kuku 15  kwa Sh 20,000 kila mmoja na kupata jumla ya 300,000, ambapo faida ya kuku na mchezo ulioendeshwa na biashara ya ndizi zilimuwezesha kuanza ujenzi.

Pesa hiyo ya 52,000 imemuwezesha kupata mtaji wa ndizi na kuku ambapo kwa pamoja zimemuwezesha kuanza ujenzi wa nyumba yake ya kudumu.

Baada ya kuanza ujenzi huo ambao mpaka sasa amefikia hatua ya kupaua, na kutengeneza chumba kimoja ambacho anaishi kwa sasa.

Akizungumzia changamoto wanazokutana nazo Antusa amesema,  pamoja na kwamba mpango huo una mafanikio makubwa lakini pia  amekutana na changamoto ikiwemo uwepo wa ugonjwa wa Covid uliosababisha kusuasua kwa malipo kutoka TASAF.

Amesema Changamoto nyingine anayokutana mayo ni zoezi la kuhamisha wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) kupelekwa kwenye maeneo maalum ambalo limemfanya kupoteaza wateja wake wa ndizi wa jumla.

Hata hivyo, Antusa ameomba kuendelea kusaidwa na Tasaf kwa zaidi ya miaka minne ili aweze kusimama mwenyewe.

Kwa upande wake, Lioba Mushi (35) mwenye nyumba watoto watatu na mume ambaye anajishughulisha na biashara ya upasuaji mbao amesema, wakati anaanza Pesa ya kwanza ya Tasaf ilikuwa Sh. 60,000 ambapo wakati anazipata alikuwa na matatizo ya kiafya na pia haikuwa na  makazi ya kudumu, alikuwa hapati chakula cha kutosha, alikuwa anakula mlo mmoja kwa siku.

Amesema gawio lake hilo la Sh. 60,000 kutoka TASAF aliligwa katika makundi matatu ambayo ni ada ya watoto, maziwa ya mtoto mchanga na Sh. 30,000 alianzisha mtaji wa kununua maparachichi ambapo kupitia fedha hizo amejiunga kwenye kikundi cha kukopeshana kwa kuchangia kati 2,000 na 5,000 biashara ambayo anaendeleana nayo mpaka leo.

Akielezea faida za mpango huo wa TASAF,  Lioba amesema,  kutokana na biashara hiyo ya  maparachichi, ameweza kujenga nyumba na kununua kondoo wawili na kujenga choo cha kisasa.

Aidha Lioba amesema, bado anautegemea sana mpango wa TASAF hivyo ameomba kupewa miezi mitatu mpaka minne ili aweze kujitegemea mwenyewe bila kusaidiwa na Tasaf.

Kwa upande wake, Mtendaji wa kata ya Uru Kusini Kitongoji cha Okaseni Kati Kijiji cha Okaseni, Severin Mende Amesema, mpaka sasa kuna kaya 520 katika vijiji sita hapo zinazonufaika na mpango wa  TASAF. 

Amesema, tangu mpango huo ulipoanza kaya mbali zimeweza kunufaika kwa kupata makazi ya kudumu na  kuondokana na changamoto ya kupata mlo mmoja kwa siku hadi milo mitatu.

Aidha amesema, mpango huo umewezesha kaya hizo kujijenga kiuchumi ambapo mpaka sasa watoto wapato 80 wameweza kupata elimu huku pia wakifanikiwa kuondoa migogoro ya familia katika kata yake.


Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...