Na Pamela Mollel,Arusha
Wanyamapori zaidi ya 200 waliokimbilia eneo la pori tengefu la mto wa Mbu yaliyopo makazi ya watu kutokana na ziwa Manyara kujaa maji na kuongezeka wadau wa uhifadhi wameanzisha zoezi maalumu la kuwakamata na kuwahamishia hifadhi jirani ya Tarangire ili kuwanusuru wanyama hao wasidhuru binadamu au wao kudhuriwa na majangili
Akizungumza na waandishi wa habari katika oparesheni hiyo inayofanyika eneo la mto wa mbu,Afisa Uhifadhi Mwandamizi tiba ya wanyamapori kutoka Tanapa Idrissa Chuma alisema zoezi la kuhamisha wanyama hao lonaendelea na tayari wameshahamisha wanyama takribani 200 kati ya 270 walioingia katika eneo hilo
"Zoezi lilianza rasmi tarehe 10/12mwaka huu tumeanza kuwakamata wanyama aina ya Punda milia na tayar tumekamata 8 kwa leo wapo ndani ya lori maalumu la kuhamishia wanyama "alisema Chuma
Alisema ili kuweza kuwakamata nilazima watumie dawa ya usingizi alafu baada ya muda huwapa dawa ya kuwazinduwa ili waweze kusimama wima kwaajili ya safari kuelekea hifadhi ya Tarangire
Pia alitaja sababu ya wanyama hao kukimbilia katika makazi ya watu ni changamoto ya ziwa kujaa maji na wanyama kusukumwa kuja katika maeneo ya makazi kutokana na eneo lao walilokuwa wakitumia kama sehemu ya malisho kuwa finyu
"Kutokana na changamoto hiyo mamlaka za usimamizi wa wanyama pori wameunganisha nguvu ya pamoja ili kunusuru wanyama hao"alisema Chuma
Wadau hao wa uhifadhi walifanya utafiti wa kina kujua idadi ya wanyama lakini pia kujua sababu za wanyama hao kutoka hifadhini na baadae waligundua sababu kubwa ni ziwa manyara kujaa maji
Hifadhi ya Tarangire inasifika sana kwa idadi kubwa ya nyumbu wanaohama kati ya Tarangire na kwenda eneo Silale mpaka Simanjiro
"Pundamilia wapo katika hifadhi ya tarangire na wanaonganishwa na shoroba na wanyama hawa vina saba vyao vinafanana"alisema Chuma
Baada ya wanyama hao kufika katika hifadhi ya Tarangire watakuwa katika uangalizi maalumu ili kujua mwenendo mzima wa wanyama hao
Mkazi wa eneo hilo wanapohamishwa wanyama hao Pascalina Daniel amepongeza zoezi hilo kwa kuwa uwepo wa wanyama hao ndani ya makazi ni hatari kwa binadamu
"Sasa hivi sisi kina mama hatuendi tena kujishughulisha tukihofia kuwaacha watoto peke yao usalama umekuwa mdogo lakini leo tumefurahi kuona wanyama hawa wanakamatwa"alisema Pascalina
Kwa upande wake mwikolojia Mkuu wa Hifadhi ya Manyara Rehema Kaitala alisema wanyama hao baada ya kukamatwa watafungwa kola maalumu kwajili ya kufatilia na kujua mwenendo mzima wa wanyama hao sambamba na kuchukua sampuli itakayowezesha kujua afya zao pamoja na kuwa na sampuli kwaajili Tafiti
Aliongeza kuwa uwepo wa wanyama hao katika makao yao mapya ya Tarangire haitawaathiri kwakuwa wanyama hao wanafanana kijenetiki
"Hapa eneo la Matete kuna mto ambao unatiririsha maji hata kipindi cha kiangazi hivyo wanyama hawatapata shida ya maji na malisho"alisema Kaitala
Naye Daktari wa wanyama na mtafiti kutoka taasisi ya wanyamapori Tawiri Dkt,Mikidadi Mtalika alisema kuwa zoezi hilo linakwenda vizuri japo linachangamoto mbalimbali ikiwemo madawa kuchelewa kufika kwa wakati
"Zoezi hili linaendeshwa kwa gharama kubwa lakini pia linahitaji muda rasilimali watu ili kufanikisha kwa wakati"alisema Mtalika
Afisa Muhifadhi Mkuu idara ya mawasiliano Tanapa Mohammed Kiganja alisema kuwa mbali na zoezi hilo kuwa na changamoto mbalimbali wao kama hifadhi wataendelea kuhakikisha wanyama wote walioingia katika makazi ya binadamu wanahamishwa na ndani ya siku 14 zoezi hilo litakuwa limekamilika
Zoezi la kuhamisha wanyama kwenda hifadhi ya Tarangire linaendeshwa na wadau wa uhifadhi Tanapa,Tawiri na Tawa
Zoezi la kuhamisha wanyama waliokimbilia eneo tengefu la mto wa mbu likiwa linaendela,wanyama hao wanahamishiwa hifadhi ya Tarangire
Afisa muhifadhi mkuu idara ya mawasiliano Tanapa Mohammed Kiganja aakieleza namna zoezi hilo litakavyohakikisha wanyamapori wote wanahamishwa kama lilivyokusudiwa
Wanyamapori aina ya pundamilia wakitoka katika lori maalumu la kuhamishia wanyama wakiingia katika makao yao mapya ya hifadhi ya Tarangire
Daktari wa wanyama na mtafiti kutoka taasisi ya Tawiri Mikidadi Mtalika akiandaa dawa maalumu zinazotumika katika zoezi la kuwakamata wanyama hao
Afisa Uhifadhi Mwandamizi tiba ya wanyamapori kutoka Tanapa Dkt,Idrissa Chuma akiongea na waandishi wa habari juu ya zoezi hilo
Mwikolojia Mkuu kutokana hifadhi ya manyara Rehema Kaitala akionyesha kola maalumu inayotumika kufatilia mwenendo mzima wa wanyama hao wakiwa katika hifadhi ya Tarangire
Mkazi wa eneo la mto wa Mmbu Pascalina Daniel apongeza zoezi hilo la kuhamisha wanyama
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...