Wakiongozwa na Wizara ya Afya kupitia Kurugenzi ya Tathimini na ubora, na Kurugenzi ya Tiba; wataalamu hao wametoa taarifa za tafiti mbalimbali zilizofanyika kwa vituo vya mafunzo vilivyokwisha anzishwa na kupendekeza njia mbalimbali za kuboresha mfumo huo wa utoaji elimu na mafunzo kwa wataalamu wa Afya nchini, pamoja na kushauri matumizi zaidi ya njia hiyo katika kipindi hiki cha majanga, ukiwemo ugonjwa wa Uviko 19.
Aidha, wameiomba Serikali kuwekeza kwenye mpango wa mafunzo ili kuwanufaisha zaidi Wataalamu wa Afya kwa kushirikiana na wadau wa nje waliobobea katika matumizi ya teknolojia katika utoaji huduma na tiba Kwa njia ya mtandao.
Kwa mujibu wa Chuo Kikuu Mzumbe watekelezaji wa Mradi huo, wameeleza kwa kushirikiana na Wizara ya Afya wamefakiwa kuanzisha zaidi ya vituo vikubwa 6 vya mafunzo na wako mbioni kufungua vingine kadhaa ili huduma ya mafunzo iweze kusambaa nchi nzima.
Msimamizi Mkuu wa Mradi CDC,Bw. Emmanuel Mtete akizungumza na wadau wa Afya kwenye mkutano wa wadau wa afya wa kutathimini mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi wa (CDC), Hennesy Nora akifafanua jambo mbele ya wadau wa Afya wakati wa mkuno wa tathimini mfumo wa mafunzo kwa njia mtandao leo jijini Dar es Salaam.
Sehemu ya wadau wa Afya kutoka sehemu mbalimbali wakiwa kwenye mkutano huo wa kutathimini mfumo wa mafunzo kwa njia ya mtandao leo jijini Dar es Salaam (Picha na Emmanuel Massaka wa Michuzi TV)
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...