Na.WAMJW-DSM 

Waziri wa Afya kutoka nchini Kenya Mhe. Mutai Kagwe awasili nchini kwa ajili ya kusheherekea maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania na kupokelewa na mwenyeji wake Waziri wa Afya Dkt. Dorothy Gwajiama.

Mara baada ya kuwasili Mawaziri hao walifanya mazungumzo ya pamoja ambapo Waziri wa Afya Dkt. Gwajima amemshukuru Mhe. Kagwe kwa kufika nchini Tanzania, ikiwa ni ishara ya kuboresha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili katika kuinua Sekta ya Afya.

Naye Mhe. Mutai Kagwe amempongeza Waziri wa Afya Dkt. Gwajima kwa hatua mbalimbali anazochukua katika kuboresha utoaji huduma za afya kwa wananchi, hususan katika eneo la mapambano dhidi ya UVIKO-19 katika kiwanja cha ndege cha kimataifa cha Julius Nyerere. 





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...