·
Mkuu wa Wilaya aipongeza kwa kuboresha huduma za
Mawasiliano
Unguja.2 Desemba 2021.Katika kuhakikisha
wateja wanapata huduma kwa urahisi, Kampuni ya Zantel imezindua duka jipya la huduma
kwa wateja lililopo michenzania Mall mjini unguja.
Uzinduzi wa duka hilo
ulifanyika jana na Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Msaraka na kushuhudiwa na
wadau mbalimbali.
Akizungumza wakati wa
uzinduzi, Mkuu wa Zantel-Zanzibar Mohammed Khamis Mussa alisema duka hilo
litasaidia kuongeza huduma za mawasiliano karibu na wateja kwani duka hilo lipo
katikati ya mji.
“Duka hili litakuwa
msaada mkubwa katika kuongeza kasi ya utoaji huduma kwa wateja wetu hapa Unguja.Eneo
hili la Michenzani ni rahisi zaidi kufikika kwa wateja wote wa maeneo ya karibu
na wanaotembelea eneo hili,” alisema Mussa.
Duka hilo ni la tatu
kwa Unguja ambapo mawili yapo maeneo ya Vuga na Mlandege.Pia, duka hilo ni la
tano kwa Zanzibar ambapo mawili mengine yapo Pemba katika eneo la Chake na
Wete.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini, Rashid Msaraka
aliipongeza Zantel kwa kuendelea kuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha
inaboresha huduma za mawasiliano visiwani Zanzibar.
“Huduma za Mawasiliano ni kiungo muhimu katika
kuchochea ukuaji wa uchumi wa nchi yetu.Zantel imekuwa mfano bora katika
kuboresha huduma za mawasiliano kwa kujenga miundombinu kama minara pamoja na
maduka kama hili tunalozindua leo,” alisema
Zantel imekuwa ikifanya uwekezaji mkubwa katika kujenga miundimbinu mipya na kuboresha iliyopo ili kuhakikisha Zanzibar yote inakuwa na Mawasiliano ya uhakika.
Hadi mwaka huu, zaidi
ya asilimia 65 ya Zanzibar ilikuwa imeunganishwa na mtandao wa 4G jambo
linalotoa fursa kwa wananchi kupata na kuzitumia fursa za kiuchumi na kijamii
kwenye ulimwengu wa kidigitali.
Hivi karibuni, Kampuni
hiyo imekuwa ikiendesha kampeni ijulikanayo kama Pasua Anga Ki Zantel 4G ambayo
ililenga kuelimisha umma juu ya umuhimu wa mtandao wa 4G kwa manufaa ya kijamii
na kiuchumi.
“Tumeona mabadiliko chanya kupitia kampeni
hii, ambapo tumeona watu wakianza kutumia mtandao kwa manufaa yao.Wapo
waliofungua biashara mitandaoni na kuongeza ubunifu kwenye kazi zao kwa kutumia
intaneti,” alisema Mussa.
Huduma
zitakazopatikana kwenye duka hilo ni pamoja na usajili wa namba za simu, bidhaa
za simu kamavile Smarta, huduma za 4G pamoja na huduma ya kifedha ya Ezypesa.
Uzinduzi wa duka hilo umekuja mara tu baada ya
kufunguliwa kwa maduka (mall) ikiwa ni fursa kwa kampuni mbalimbali kusogeza
huduma karibu na wateja wao.
Mkuu wa Wilaya ya Mjini-Unguja, Rashid Msaraka akikata utepe kuzindua duka jipya la Zantel lililopo eneo la biashara la Michenzani Mall.Kulia ni Mkuu wa Zantel-Zanzibar Mohammed Khamis Mussa na Emmanuel Joshua, Mkuu wa Mauzo, Usambazaji na Huduma kwa wateja.Duka hilo ni la tatu kwa Unguja na la tano kwa Zanzibar litakalosaidia kusogeza huduma karibu na wateja.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...