Na Amiri Kilagalila,Njombe
Tyson Kilasi (32) mkazi wa kijiji cha Mawindi halmashauri ya wilaya ya Wanging’ombe mkoani Njombe,amekutwa amefariki kwa kujinyonga kwenye goli la kuchezea mpira wa miguu wa kijiji hicho huku pembeni akiwa ameacha nguo ya ndani ya kike.
Mwenyekiti wa kijiji cha Mawindi kata ya Igima bwana Elias Mwinami amethitibitisha kutokea kifo cha kijana huyo kilichotokea usiku wa kuamkia January 18.
Bwana Mwinami amesema chanzo cha kifo cha kijana huyo bado hakijafahamika ambapo eneo ambalo mwili wa kijana huyo wameukuta ni eneo la goli la mpira wa miguu na wamekuta nguo ya ndani ya mwanamke.
“Tumemkuta asubuhi ananing’inia kwenye goli lakini chanzo bado hakijafahamika na kimsingi tunalaani kitendo hiki ifike mahali tuelimike na hivi karibuni tu pilisi walikuja kutoa elimu kwa kweli wananchi waache kujichukulia sheria mkononi”alisema Mwinami
Akizungumza kwa njia ya simu Diwani wa kata ya Igima bi. Paulina Samata Mwinami amesema kata ya Igima inahitaji juhudi za pamoja kuelimisha wananchi juu ya kuacha kujichukulia sheria mkononi na kwamba tukio hilo ni la pili kutokea kwenye kata hiyo.
Bi.Mwinami amesema wiki moja imepita mwanaume mmoja na mwanamke mmoja walikutwa wameuawa katika misitu ya kampuni ya Tanwat ambao walitambulika kuwa ni wakazi wa kata ya Igima mmoja wa kijiji cha Mawindi na mwingine mkazi wa kijiji cha Mhaji ambao uchunguzi wa polisi bado unaendelea.
“Nilivyojaribu kuuliza kama jana ulitokea ugomvi wamesema hawaelewi kwa kweli ninajiskia vibaya mno kwasababu watu sasa wanajichukulia sheria mkononi.Niombe wananchi kama wanakuwa na kitu ni vema wawe wanakitoa kuliko kuchukua uamuzi wa kujiua”alisema Paulina Samata
Baadhi ya wananchi na majirani wa marehemu huyo wamesema serikali iongeze kasi ya kuelimisha wananchi kupitia mikutano ili kupunguza matukio ya vifo katika kata hiyo na kwamba migogoro katika familia, ardhi na uhusiano wa kimapenzi ndiyo inayohisiwa kuwa chanzo cha matukio hayo.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...