Na John Walter-Manyara
Si jambo la kawaida mzazi kuwa na uhusiano na mtoto wake wa kumzaa, na jamii nyingi zimekuwa zikipinga na kukemea maovu ambayo hufanywa na baadhi ya wazazi kuwafanyia vitendo vya unyanyasaji watoto wao hasa wale ambao hata hufikia hatua ya kubaka binti zao.
Kuna hii imetokea katika wilaya ya Kiteto mkoani Manyara ambapo inadaiwa baba kambaka binti yake wa miaka 15 mwanafunzi wa darasa la saba akiwa chumbani kwake.
Jeshi la Polisi mkoani Manyara limethibitisha kutokea kwa tukio hilo ambpo Kamanda wa Jeshi hilo mkoani hapo Benjamin Kuzaga amesema limetokea Januari 11,2022 katika kijiji cha Ndareta kata ya Njoro.
Kuzaga amesema vipimo vya daktari vimebaini ni kweli mwanafunzi huyo amefanyiwa kitendo hicho na kwamba inavyoonekana ni kawaida kwa mtuhumiwa kumbaka mtoto wake akiwa amelewa.
Hata hivyo Jeshi hilo kwa kushirikiana na wananchi limefanikiwa kumkamata mtuhumiwa na kwamba taratibu za kumfikisha katika vyombo vya sheria zinaendelea.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...