Adeladius Makwega-WUSM

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Innocent Bashungwa (MB), amefanya uteuzi wa wajumbe 12 wa Kamati ya Tamasha la Serengeti (Serengeti Music Festival) chini ya uenyekiti wa Mkurugenzi wa Maendeleo ya Sanaa nchini Dkt. Emmanuel Ishengoma.

Uteuzi huo wa Waziri Bashungwa una wajumbe wanne kutoka vyombo vya habari nchini ambao Mkuwe Isale kutoka Clouds Media Group, Hamis Mandi kutoka EFM, Omary Tambwe kutoka Wasafi na Tatenda Nyawo wa A FM Radio ya Dodoma.

Taarifa hiyo iliyotolewa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na Michezo Dkt. Hassan Abbasi imewataja wajumbe wengine ni Paschal Shelutete ambaye ni Afisa kutoka Mamlaka ya Mbuga za wanyama nchini (TANAPA), Hamza Shareeph wa Tigo Tanzania na Addo Novemba ambaye ni Rais wa Shirikisho la Muziki Tanzania.

Wajumbe wengine wanne ni watatu wanatoka taasisi za mabenki ya hapa nchini ambao ni Neema Singo wa NBC, Jadi Ngwale wa CRDB na Mercy Nyange wa NMB na Katibu wa Kamati ya Tamasha la Serengeti Mniko Matiko, ambaye ni Kaimu Katibu Mtendaji Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA).

“Uteuzi wa wajumbe wa kamati hiyo utasaidia kuratibu tamasha hilo la kitaifa lenye dhima ya kuwaleta wasanii pamoja na ni muunganiko na tukio la kimkakati la sekta za sanaa na utalii katika kuitangaza nchi yetu.” Alisisitiza Waziri Bashungwa.

Mheshimiwa Bashungwa huku akiwatakiwa heri na fanaka za mwaka mpya wa 2022 wadau wote wa Utamaduni, Sanaa na Michezo nchini amesema kuwa kamati hii inaanza utekelezaji wa majukumu yake kwa kushirikiana na waratibu wa tamasha hilo mara moja.







Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...