Benki ya Exim Tanzania imetangaza washindi wa promosheni yake inayojulikana kama “Weka Mkwanja tukutoe!” ambapo taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliibuka mshindi wa zawadi kuu gari aina ya Toyota Vanguard kwenye kampeni hiyo iliyolenga kuhamasisha wateja wake kujiwekea akiba.

Mbali na taasisi hiyo washindi wengine sita (6) waliweza kujishindia zawadi ya fedha taslimu mil 1 kila mmoja katika droo hiyo iliyofanyika makao makuu ya benki hiyo jijini Dar es Salaam kwa usimamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha nchini pamoja na wawakilishi wa vyombo vya habari pamoja na maofisa mbalimbali wa benki hiyo.

Washindi waliojinyakulia zawadi ya fedha taslimu ni pamoja na Didas Patrick Moshi, SN Partners Architects Limited, Amirali Hassanali Alarakhia/Tahir Amir Alarakhia, Fatna Saleh Tambwe, Stewart Emmanuel Kinunda na Peter Tulizo Sewa ambao walizawadiwa fedha kiasi cha sh Mil 1 kila mmoja.

Akizungumza wakati wa droo hiyo, Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo alisema kupitia kampeni hiyo mbali na gari hiyo jumla ya fedha kiasi cha sh mil 18 zilitolewa kwa washindi wapatao 18 ambapo pia benki hiyo imeweza kuongeza mtandao zaidi wa wateja wapya huku pia ikifanikiwa kuhamasisha wateja waliokuwepo awali kujiwekea akiba zaidi.

“Katika promosheni hii iliyodumu kwa kipindi cha miezi mitatu, wateja wetu wa awali na wale wapya waliofanya miamala kuanzia kiasi cha sh laki tano (500,000) na kuendelea, waliweza kuingia moja kwa moja kwenye droo kubwa ya kujishindia gari yaina Toyota Vanguard pamoja fedha taslimu kiasim cha sh mil 1 kila kwa kila mshindi,’’

“Huu ulikuwa ni muendelezo wa utamaduni wa benki ya Exim katika kutoa zawadi bora na faida kwa wateja wetu huku wakati huo huo tukiendelea kutoa huduma bora za kibenki.’’ Alisem Lyimo.

Kwa mujibu wa Bw. Lymo kampeni hiyo ya “Weka mkwanja tukutoe” haikuwasaidia tu wateja wao kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba bali pia imewazawadia kwa jitihada hizo.

“Tunafurahia kuwazadawadia washindi wa promosheni ya“Weka mkwanja tukutoe” na matumaini yetu kuwa watawavutia wengine kuanza kujijengea utamaduni wa kujiwekea akiba. Tutaendelea kujenga tabia ya kuweka akiba nchini ambapo tutawasaidia wateja wetu kutimiza malengo ya muda mrefu na mfupi kwa kujiunga na benki yetu” alisema.

Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo (Katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa zoezi la uendeshaji wa droo kubwa ya kuwatafuta washindi kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ ambapo taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliibuka mshindi wa zawadi kuu gari aina ya Toyota Vanguard kupitia kampeni hiyo wakati wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ikilenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kujiwekea amana kupitia benki hiyo. Wengine ni Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu (Kushoto) na Ofisa kutoka Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Bw Elibariki Sengasenga (Kulia).


Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu (katikati) akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani ) wakati wa zoezi la uendeshaji wa droo kubwa ya kuwatafuta washindi kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ ambapo taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliibuka mshindi wa zawadi kuu gari aina ya Toyota Vanguard kupitia kampeni hiyo wakati wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ikilenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kujiwekea amana kupitia benki hiyo. Wengine ni Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo (Kulia) na Meneja Msaidizi wa Bidhaa za Rejareja kutoka benki hiyo, Callist Butinga (Kushoto)


Wafanyakazi wa Benki ya Exim wakiwemo Mkuu wa idara ya wateja wadogo na kati Benki ya Exim Bw Andrew Lyimo (wa pili kulia) pamoja na Mkuu wa Idara ya Masoko na Mawasiliano wa Benki hiyo Bw Stanley Kafu (wa pili kushoto) wakifuatilia uendeshwaji wa droo kubwa ya kuwatafuta washindi kampeni ya ‘Weka Mkwanja Tukutoe!’ ambapo taasisi ya Work of Mary (Focolare Movement Tanzania) ya mkoani Iringa iliibuka mshindi wa zawadi kuu gari aina ya Toyota Vanguard kupitia kampeni hiyo wakati wa droo iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo ikilenga kuhamasisha wateja wa benki hiyo kujiwekea amana kupitia benki hiyo.





Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...