Na Chalila Kibuda,Michuzi TV

Mwanasiasa Mwandamizi Danda Juju amesema Bunge ni mhimili unaoaminika hivyo ikitokea mtu yeyote inapotokea amekwenda tofauti kwenye nafasi ya Spika anatakiwa kujiuzulu ili chombo hicho kiendelee kuheshimika na Watanzania.

Kauli hiyo imekuja hivi Karibuni baada ya Spika Job Ndugai kuzungumzia juu mikopo ya nchi ambapo aliweza kuomba msamaha lakini haitosho anatakiwa kujiuzulu.

Danda amesema Spika Job Ndugai ana uwezo mkubwa katika kutumikia bunge katika nafasi mbalimbali lakini kwenye hili amewakosea watanzania.

Amesema kuwa chombo cha Bunge kinategemewa kwa kutunga sheria hivyo ikitokea Spika anazungumza jambo ambalo mwisho wa siku linaleta taharuki lakini mwisho wa siku anaomba radhi hilo haliko sawa.

Amesema kuwa kuendelea kuwepo kwa Spika Ndugai katika kiti hicho haileti afya kuheshimia kwa chombo cha bunge.

Danda amesema hapa kilichotokea sio kumuonea wivu katika nafasi bali kufanya chombo cha Bunge kiindelee kuheshimika ili aistokee mtu mwingine kufanya hivyo.

Danda amesema kuwa Spika alikuwa na uwezo wa kukutana Rais na kuzungumzia hilo lakini alishindwa kufanya hivyo na kutumia njia nyingine ya kufiksha ujumbe.

Aidha Danda amesema kuwa Spika kwa nafasi yake aliona mikopo katika serikali zote lakini hakusema katika kipindi kifupi cha Rais Samia Suluhu Hassan anakuja kuzungumza watanzania wanashindwa kuelewa.

Kada wa CCM Danda Juu (Pichani kulia) akiwa na fomu ya kugombea Ubunge Jimbo la Njombe Mjini 2015

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...