Mkuu wa Wilaya ya Muheza Mkoani Tanga Halima Bulembo amewataka Wazazi na Walezi wilayani humo kuhakikisha wanawapeleka watoto wao wenye umri wa kuanza shule pindi zitakapofunguliwa Januari 17 mwaka huu.
Pia amesema kwa Mzazi yoyote atakayeshindwa kumuandikisha na kumpeleka mtoto wake shule hatua Kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yake.
Wito huo ameutoa wakati wa ziara yake ya kuhamasisha maendeleo na uandikishwaji wa watoto wa darasa la kwanza ambapo kwa nchi nzima jumla ya Watoto 1,581,823 wanatarajiwa kuanza darasa la kwanza mwaka 2022.
Bulembo alisema kuwa Rais Samia ameshafanya kipande chake kwa kujenga Madarasa katika kila kata nchi nzima sasa ni muda wa wazazi kufanya kipande chao kuhakikisha wanafunzi wote wanaandikishwa ili shule zitakapofunguliwa waanze shule.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya huyo ameahidi kupita Kijiji kwa Kijiji ili kuhamasisha Wazazi kuwapeleka shule watoto wao.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...