Ikiwa imesalia siku moja kufunguliwa kwa shule nchini,Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) limetangaza matokeo ya mitihani ya darasa la nne, kidato cha pili na kidato cha nne



Mara baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Shule Binafsi zimeendelea kushika nafasi za juu katika matokeo hayo na shule ya Feza ikiingia katika kumi bora mara 3

Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar,Mkurugenzi wa shule za Feza nchini, Ibrahm Yunus alisema wao katika matokeo haya wameyapokea vizuri kutokana na kutimia kwa malengo yao waliojiwekea mwaka uliopita ya kuhakikisha wanaendelea kuwamo katika kumi bora.

Akifafanua Zaidi alisema ushindani wa shule umekuwa mkubwa sana ndio maana miaka ya hivi karibuni shule nyingi zimekuwa zikiingia katika kumi bora na kutoka.

Pia alisema wao wamefanikiwa kuingiza wanafunzi wa 2 katika kumi bora kwa upande wa wavulana Feza Boys (7)na wasichana Feza Girls (9) hivyo ni hatua ya kujivunia kama shule .

Kwa upande wa wanafunzi , Imam Mogaeka akielezea siri ya mafanikio amesema ni kujituma na kusikiliza maagizo ya waalimu awapo shuleni na wazazi pindi arudipo nyumbani na kupata muda mwingi wa kujisomea, ndio, silaha ya matokeo mazuri

Akimalizia Mwalimu wa taaluma wa shule ya Feza Boys , Saimon Albert alisema UTATU Mtakatifu ndio silaha yao katika kufundisha na akimaanisha Mzazi ,Mtoto na Mwanafunzi muunganiko wa maelewano ya utatu huu ndio hupelekea matokeo mazuri tulikubaliana na wazazi kuwa wanafunzi wanatakiwa kusoma wakati wote bila kujali yupo shule au nyumbani hali ambayo wazazi walituelewa na hatimae matunda yake yanaonekana Pia kuna kipindi tulianzisha slogani ya hakuna kulala mpaka kieleweke yaani mwanafunzi anasoma na analala na vitabu kitandani tunashukuru mungu leo tupo vizui.


Mkurugenzi wa shule za FEZA nchini, Ibrahm Yunus akizungumza na Waandishi wa habari baada ya matokeo ya kidato cha nne na cha pili kutangazwa na shule yao kushika nafasi ya saba Kitaifa huku wanafunzi wawili wakiingia kumi bora.Kulia ni mkuu wa shule ya wasichana, Zakia Irembe na Kushoto ni mtaaluma wa shule ya wavulana, Saimon Albert.

Mwanafunzi wa kidato cha nne shule ya Feza Boys, Imam Mogaeka na mwenzake wakipongezwa na waalimu baada ya kufanya vizuri katika matokeo ya kidato cha pili na cha nne katika matokeo ya mitihani yaliotangazwa jijini Dar es salam leo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...