BAADA ya Miongo mingi ya Utayarishaji wa muziki, kurekodi, Na kupiga gitaa katika Nyimbo nyingi Za wasanii wa Afrika, Fiokee ameuanza mwaka Kwa kuachia Albamu yake “MAN”.

Ambapo albamu hiyo amemshirikisha msanii kutoka Tanzania “MAUA SAMA pamoja na Yemi Alade kutoka Nigeria Ni miongoni mwa wasanii walioshirikishwa.

MAN, Fiokee amedhihirisha kuwa yeye tu sio mpiga gitaa bali anaweza kufanya Vitu vingi ingawa pia Ni mtayarishaji mzuri wa muziki. 

Albamu hii ya Fiokee inaonyesha Ni kiasi gani Ana uwezo wa kutengeneza muziki mzuri unaoweza kuishi, na ameitoa albamu hii Kama Zawadi kwa mashabiki katika Huu mwaka anaotimiza miaka 40 ya kuzaliwa. 

Pia unaweza kuisikiliza sasa kupitia Platforms zote zinazouza na kusikiliza muziki Duniani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...