*Aungana na Rais Kwenye mikopo ya maendeleo na asife Moyo
Na Chalila Kibuda,Michuzi TV
Askofu Josephat Gwajima amesema kuwa yeye hayuko na Sukuma Gang katika hili kwa busara imuongoze kujiuzulu kusahamewa sio suluhisho.
Gwajima ameyasema hayo leo wakati akizungumza na waandishi wa habari amesema kuwa Spika Ndugai ni boss wake lakini kwenye hili amepoteza heshima ya chombo cha Bunge kwani Spika sio lazima awe mwanachama wa chama cha Mapinduzi.
Gwajima amesema kuwa Suala la Mkopo lilipita katika kamati ya Bunge ya Fedha na Mipango lakini anashangaa hakuhoji katika kamati hiyo na kuibuka baada ya mwezi moja na zaidi.
Amesema anaungana na Rais Samia Hassan Suluhu kwa kuwa mkopo huo umekuwa na manufaa kutokana na mgawanyo wa fedha katika ujenzi wa vyumba vya Madarasa.
Amesema wakati akizunngumza alimtumia kuwa Spiker I know ambaye hiyo ina maana nyingi na sio kukubaliana na hoja yake aliyezungumza na kuongeza kuwa haijiuzulu.
Amesema kuwa kutokana na kauli ya Spika Mh.Rais Samia Hassan Suluhu inamnyong'osha katika utafutaji wa fedha hivyo ajiuzulu.
Amesema kila Rais amekuwa akikopa na hivyo sio sawa kubebeshwa mzigo wa mikopo Rais Samia Hassan Suluhu kana kwamba yeye ni wa kwanza kuanza kukopa.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...