NA YEREMIAS NGERANGERA…NAMTUMBO.
Kikao cha baraza la ushauri Mkoa wa Ruvuma kilifikia maamuzi ya kuunda tume kufuatilia mienendo ya makampuni yanayotekeleza miradi ya umeme vijijini REA kusuasua katika utekelezaji wake hali inayoleta kero kwa wananchi katika mkoa wa Ruvuma .
Wakiongea katika kikao hicho mbunge wa Tunduru kusini Daimu Mpakate alimwomba mkuu wa mkoa wa Ruvuma kuwaita wakandarasi wanaosimamia utekelezaji wa umeme vijijini REA kujiridhisha na sababu inayosababisha kusuasua kwa utekelezaji wa miradi ya umeme vijiji katika mkoa wa Ruvuma .
Mbunge wa madaba Joseph Mhagama kwa upande wake alidai maamuzi magumu ya kuwakataa wakandarasi wanaochelewesha utekelezaji wa miradi unahitajika kwani bila kufanya hivyo utekelezaji wa miradi haufanyiki kwa wakati .
Mhagama alitolea mfano wa mkandarasi aliyekuwa anasimamia mradi wa maji jimboni kwake kuwa walichukua maamuzi magumu ya kumsimamisha na mkandarasi aliyepewa yupo saiti anachapa kazi hali iliyoondoa malalamiko kwa wananchi kwa kuwa wananchi kwa sasa wanamwona mkandarasi hatua kwa hatua kazi anazozifanya na kuondoa malalamiko tofauti na yule aliyesimamishwa na kushauri baraza kuchukua maamuzi magumu ya kuwasimamisha wakandarasi wanaokwamisha miradi ya umeme vijiji REA.
Juma Pandu mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Namtumbo alikiomba kikao hicho kutafuta mbinu mbadala ya kuwafanya wakandarasi hao wafanye kazi zao kwa haraka badala ya kuvunja mkataba kwa kuwa watawasababishia hasara kubwa wakandarasi hao lakini pia itachukua muda mrefu tena wa mchakato wa kuwapata wakandarasi wengine na wakati mwingine kupelekana mahakamani .
Mhandisi Stella Manyanya Mbunge wa Nyasa alishauri kabla ya kuvunja mkataba kikao kinatakiwa kijiridhishe sababu ya wakandarasi wa miradi ya umeme vijijini REA wanakumbana na changamoto ipi ambayo inaweza kuwa ndiyo inayosababisha miradi kuchelewa na changamoto hizo zinaweza zikawa sio za mkandarasi ni za mwenye kutoa kazi hivyo inatakiwa kulishughulikia jambo hilo kwa busara kubwa alisema Manyanya.
Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Ruvuma Oddo Kirian Mwisho pamoja na mambo mengine aliwaambia wajumbe wa baraza la ushauri la mkoa kuwa chama kilimwomba mkuu wa mkoa kuwaita wakandarasi wanaotekeleza miradi ya umeme vijijini REA baada ya kamati ya siasa mkoa kupita katika wilaya kufuatilia utekelezaji wa ilani na kukumbana na malalamiko makubwa kutoka kwa wananchi kuhusu kusuasua kwa miradi ya umeme vijiji REA.
Mwisho alidai wakati wa kikao cha mkuu wa mkoa na wakandarasi hao hakuna mkandarasi aliyedai anashindwa kutekeleza mradi kwa sababu anadai fedha, zaidi ya kuhaidi kufanya kazi kwa kuongeza kasi zaidi lakini hali bado ni ileile alisema mwenyekiti wa chama mkoa Oddo Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma Brigedia Generali (Balozi) Wilbert Ibuge baada ya kupokea maombi na ushauri wa wajumbe kuhusu azimio la kuunda tume ya kuchunguza sababu ya kusuasua kwa miradi ya umeme vijiji Rea aliridhia azimio la kuunda tume itakayofanya ufatiliaji na kutoa mapendekezo kwake kabla ya tarehe 20 mwezi machi 2022.
Kikao cha baraza la ushauri la mkoa wa Ruvuma kilifanyika hivi karibuni katika ukumbi wa manispaa ya songea kilichotanguliwa na maombi ya mvua na kisha kujadili mambo ya maendeleo yanayohusu mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...