Katibu Mkuu wa Utamaduni, Sanaa na Michezo. Dkt Hassan Abbasi amesema Serikali kupitia Baraza la Sanaa la Taifa ( BASATA) inakwenda kuweka wazi vigezo vya tuzo za muziki ili wasanii waweze kushiriki kikamilifu na kushinda tuzo za miziki ambazo Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo imefufua   sasa baada ya miaka saba kupita bila tuzo hizo.

Dkt. Abbasi amesema hayo leo alasiri Januari 28, 2022 kwenye kipindi cha XXXL kilichorushwa mbashara kuhusu Uzinduzi wa Tuzo za Muziki na Ugawaji  wa mirabaha  kwa wasanii unaofanyika usiku wa leo Januari 28,2022 kwenye Ukumbi wa Kimataifa  wa  Julius Nyerere jijini Dar es salaam.

Mgeni rasmi kwenye hafla hiyo ni Waziri mwenye dhamana ya Sanaa nchini Mohamed Mchengerwa ambapo wadau mbalimbali wa Sanaa na vikundi mbalimbali vya wasanii vimealikwa kutumbuiza kwenye hafla hii inayokwenda kwa jina la#2 KUBWA ZA2022.

Ameongeza kuwa baada ya kuweka wazi vigezo hivyo mtandaoni  zitafuata warsha za uelimishaji kwa wasanii.

Amesema kilele cha utoaji wa tuzo hizo utakuwa Machi 26, 2022 ambapo ametaja baadhi ya vigezo vya jumla vya kuzingatia ni kuwa washiriki lazima wawe watanzania.

Vigezo vingine ni lazima kuthibitisha umiliki wa kazi hiyo na kazi hiyo iwe imetoka  ndani ya kipindi cha mwaka 2021.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...