Pamela Mollel – Arusha

Tanzania imeanzisha aina mpya ya utalii wa kutumia magari ya zamani au ‘Classic Cars!’

Utalii huu mpya unaanza rasmi mwaka huu wa 2022 na utakuwa unafanyika mara mbili kwa mwaka katika hifadhi za taifa.

Tayari majaribio ya awali yamefanyika katika hifadhi ya Arusha ambako magari takriban 17 yameweza kufanya utalii huo maalum.

Kamishna wa uhifadhi kanda ya kaskazini Herman Batiho amesema kuwa hifadhi ya Arusha iliyoanzishwa mwaka 1960 ni ya pili yenye umri mkubwa baada ya Serengeti.

“Ndio maana tumeichagua kwa sababu kuna magari ambayo yalikuwa yakitumika katika shughuli za utalii kipindi hicho cha mwaka 1960 ambayo yapo hapa leo,” alisema Batiho. 

Miongoni mwa magari yaliyozindua aina hii mpya ya utalii ni pamoja na Volkswagen Kobe au beetle ya mwaka 1968, Landrover 108 na 109 pamoja na Landcruiser za miaka ya 60 na 70.

Mkuu wa hifadhi ya Arusha Albert Mziray, amesema kuwa magari hayo ya zamani yatasaidia kujenga taswira mpya ya utalii eneo hilo ambalo awali lilitumika kutengeneza filamu iitwayo Hatari ambayo pia ilihusisha magari ya zamani.

“Tunatarajia kufanya aina hii ya utalii mara mbili kwa mwaka, ingawa tayari tuna utalii mwingine wa kutumia usafiri wa farasi hifadhini,” alisema Mziray.

Sady Mnene ni mmoja wa washiriki wa utalii huo, akiendesha landrover 109.

“Nimeanzisha utaratibu wa kuyafufua na kuyarekebisha magari ya zamani ambayo kwa sasa yana thamani kubwa na watu huyatafuta kwa wingi,” alisema Mnene.

Mwingine ni Edson Sengiyuva akiendesha Volkswagen Beetle ambaye anasema hupendelea zaidi magari ya kampuni hiyo na kwamba alikuwa pia na VW Kombi maalum kwa utalii.

Elfride Aikaniwa ni mwanamke pekee aliyeshiriki utalii huo wa magari ya zamani akiendesha Toyota Landcruiser FJ40. Anasema kuwa yeye hupenda gari hilo sio tu kwa utalii bali hata katika matumizi yake ya kila siku.

Kamishna wa uhifadhi kanda ya kaskazini Herman Batiho katikati mwenye koti la suti, akifungua rasmi aina mpya ya utalii wa kutumia magari ya zamani katika hifadhi ya Arusha National Park mwenyewe  suti ya blue anayepiga makofi ni Mkuu wa hifadhi ya Arusha Albert Mziray

Magari ya zamani yakiwa katika hifadhi ya Arusha National park ikiwa ni aina mpya ya utalii wa magari ya zamani

Elfride Aikaniwa ni mwanamke peeke aliyeshiriki utalii wa magari ya zamani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...