MIPANGO NA DHAMIRA NJEMA CHACHU YA KUFIKIA MAFANIKIO - MHE. OTHMAN

MJUMBE wa Kamati Kuu cha Chama Cha ACT- Wazalendo Mhe. Othman Masoud Othman, amesema wanawake wenye upeo wa kubuni na kutekeleza program na mipango mbali mbali ya chama ni mtaji na hazina kubwa ya chama chochote cha Siasa.

Mhe. Othman  ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar ,ameyasema hayo leo Januari 26, mara baada ya kuzindua rasmi Kadi ya Wanawake ya Chama hicho huko katika Hoteli ya Lamada,Ilala mjini Dar es Salaam.

Amesema kuwepo wanawake wa aina hiyo ni muhimu katika juhudi za kujenga na kuimarisha chama, kwa vile watabuni na kutekeleza mipango na program mbali mbali ambazo watazisimamia wenyewe kwa ufanisi.

Mhe. Othman  aliyeambatana na mke wake Mama Zainab Kombo Shaib, sambamba na kuwapongeza wanawake wa chama hicho kwa kuwa wabunifu na kuonesha uwezo mkubwa katika kuendesha mipango yao, pia amewataka kusimamia dhamira ya kweli katika umoja na mshikamano ili kuyafikia malengo ya Chama hicho.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya Chama cha ACT-Wazalendo amewasili mjini Dar es Salam kushiriki vikao mbali mbali  vya Chama ikwemo Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano mkuu wa Chama hicho, unaotarajiwa kufanyika Januari 29.

Naye  Mjumbe wa Kikosi kazi cha Ngome ya Wanawake wa  Chama hicho Bi. Severina Mwijage, amesema kwamba Chama chao kimeamua  kuanzisha kadi ya wanawake wa chama hicho kwa dhamira ya kuongeza ushajihishaji na ushiriki zaidi wa wanawake katika harakati za kujenga chama.

Mjumbe wa Kamati Kuu cha Chama Cha ACT- Wazalendo,ambayepia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Mhe. Othman Masoud Othmanakizindua  kadi ya uwanachama wa Mwanamke wa ACT Wazalendo katika Hoteli ya Lamada Dar es salaam (picha Ofisi ya Makamu wa kwanza)

Mjumbe wa Kamati Kuu cha Chama Cha ACT- Wazalendo,ambayepia ni Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar,Mhe. Othman Masoud Othman, akizungumza na wanachama wanawake wa chama hicho mara baada ya Uzinduzi wa kadi ya uwanachama wa Mwanamke wa ACT Wazalendo katika Hoteli ya Lamada Dar es salaam (picha Ofisi ya Makamu wa kwanza)

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...