Mwanasheria Mkuu wa Mhe. Jaji Dkt Eliezer Feleshi jana (jumanne) ameongoza ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Wanasheria Wakuu na Mawaziri wa Sheria wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika ( SADC)
Mkutano huo ulifanyika katika Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa njia ya mtandao .
Pamoja na mambo mengine wajumbe wa mkutano huo wamepitisha mabadiliko ya Ibara ya 9 ya Mkataba wa uanzishwaji wa Jumuiya ( SADC Treaty) kwa kuongeza Bunge la SADC ili kuipa mamlaka Jukwaa la Bunge la SADC kuwa Bunge Kamili.
Vile vile Mkutano huo pia umepitisha Mkataba unaofanya mabadiliko katika Itifaki ya Utalii ( Draft Agreement amending SADC Protocoal on development of Tourim) na Kanuni za Dhamana ya usafirishaji wa mizigo katika Kanda ( Revised Regional Customs Transit Gurantee Regulations).
Katika Mkutano huo, Mwanasheria Mkuu aliambatana na wataalamu kutoka Ofisi ya Mwanasheria Mkuu , Ofisi ya Waziri Mkuu, Afisi ya Rais Zanzibar, Wizara ya Katiba na Sheria, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushrikiano wa Kimataifa, Wizara ya Fedha, Wizara ya Maliasili na Utalii na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Nchi wanachama walioshiriki mkutano huo kwa njia ya mtandao ni Angola, Botswana, Congo, Eswatini, Lesotho,Mozambique, Madagascar,Nambia, South Afrika, Zambia, Zimbabwe na Tanzania
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...