Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na marehemu kaka yake Askofu Mstaafu Gerald Mpango tarehe 16 Desemba 2021 wakati Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoani Kigoma. Askofu Mstaafu Gerald Mpango alifariki jana tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam.



MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango amefiwa na kaka yake Askofu Mstaafu wa Kanisa la Anglikana Tanzania Gerald Mpango. 

Askofu Gerald Mpango amefariki tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 

Enzi za uhai wake Askofu Gerald Mpango alihudumu katika kanisa la Anglikana Dayosisi ya Magharibi ya Tanganyika ( Diocese of Western Tanganyika) Mazishi ya Askofu Mstaafu Gerald Mpango yanatarijiwa kufanyika siku ya Jumamosi tarehe 22 Januari 2022 wilayani Kasulu Mkoani Kigoma.

Mazishi hayo yatatanguliwa na ibada ya kuaga mwili wa marehemu itakayofanyika katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Albano lililopo Posta Jijini Dar es salaam siku ya Ijumaa tarehe 21 Januari 2022.

Baadaye mwili utasafirishwa kwenda mkoani Kigoma kisha kufuatiwa na Ibada ya kuaga mwili huo katika kanisa la Anglikana la Mtakatifu Andrea Kasulu Kigoma.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akizungumza na ndugu, jamaa na marafiki mbalimbali waliofika nyumbani kwa marehemu Askofu Mstaafu Gerald Mpango Boko Jijini Dar es salaam. Marehemu Askofu Mstaafu Gerald Mpango ni kaka wa Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango. Januari 20,2022.



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na marehemu kaka yake Askofu Mstaafu Gerald Mpango tarehe 16 Desemba 2021 wakati Makamu wa Rais alipofanya ziara mkoani Kigoma. Askofu Mstaafu Gerald Mpango alifariki jana tarehe 19 Januari 2022 Jijini Dar es salaam.





 

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...