Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Philip Mpango hii leo tarehe 10 Januari 2022 anaondoka nchini kuelekea Lilongwe nchini Malawi kumuwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan katika Mkutano wa Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi wananchama wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini Mwa Afrika (SADC) utakaofanyika tarehe 12 Januari 2022.
Mkutano huo utatanguliwa na Mkutano wa
Dharura wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Asasi ya Ushirikiano katika Masuala ya
Siasa , Ulinzi na Usalama (Organ Troika Summit) utakaofanyika tarehe 11 Januari
2022.
Franco Singaile
MMR – Habari.
Januari 10,2022.
Toa Maoni Yako:
0 comments so far,add yours
Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...