Na.Khadija Seif Michuzi TV

Imeelezwa kuwa UJIO wa Mpishi wa Kimataifa umelenga kuwanufaisha na kutanua wigo wa Masoko ya Waokaji Vitafunwa pamoja na Keki ndani na nje ya nchi mbalimbali.

Akizungumza na Michuzi Muandaaji wa Tamasha la Waokaji ambae pia ni Mmoja ya wanakamati katika Tamasha kubwa la darasa la Mapishi Kwa vitendo ,Manka Rajab amesema ujio wa Mpishi huyo wa Kimataifa chief Tuba utakua na Manufaa makubwa sana Kwa wajasiriamali hususani Kwa wapishi hao wavitafunwa na keki .
"Ni Mpishi ambae anazunguka nchi mbalimbali Kwa ajili ya kutoa Mafunzo namna ya kutengeneza keki Kwa maumbo tofauti tofauti hivyo kwetu sisi wapishi tutaweza kutengeneza vitu ambavyo Kwa Sasa hapa Tanzania pengine havijaonekana au Vinaweza kuwepo lakini vinahitaji marekebisho Kwa kiasi Fulani Ili tutengeneze vitu Kwa weledi unaohitajika."

Pia Manka amempongeza Muandaaji wa Darasa hilo Zena Sharif Kwa kuona ipo fursa kwake kumleta Mpishi huyo wa Kimataifa nchini Tanzania na kuunganisha nchi zilizokaribu kuweza kushiriki darasa hilo Kwa siku kadhaa.

"Darasa hilo litaanza rasmi januari 17 mpaka 22 ikifatiwa na chakula Cha usiku pamoja na Mpishi huyo na tunategemea kuwepo Kwa viongozi kutoka Serikalini hii inaonyesha sisi kama wapishi tunathaminiwa ukizingatia wengi wetu bado ni walezi wa familia zetu ( Single Mothers) ."

Hata hivyo Manka amesema katika darasa hilo litajumuisha wapishi wa ndani na nje ya nchi kwani mpaka Sasa wameshalipia tiketi Kwa ajili ya ushiriki wao .
Mpishi wa Kimataifa Chief Tuba ambae anatarajiwa kufika nchini Tanzania Kwa lengo la kutoa Mafunzo jinsi ya Kutayarisha Keki na pichani akionesha Moja ya Keki ambayo imetengenezwa Sura ya Mchezaji wa Mpira nchini Brazil Neymar

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...