Na Said Mwishehe, Michuzi TV

KADA wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Hanang mkoani Manyara, Mhandisi Samwel Hhayuma, amerejesha Fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea nafasi ya Uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, leo Januari 15, 2022, katika ofisi ndogo za CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.

Akizungumzia na waandishi wa habari leo Januari 15 katika Ofisi ndogo za  CCM zilizopo Lumumba jijini Dar es Salaam Mhandisi Hhayuma amesema baada ya kurejesha fomu hiyo anasubiri mchakato wa ndani ya Chama kwa ajili ya kupata ridhaa ya kuwania nafasi hiyo.

Kuhusu  kujitokeza kwa watu wengi katika hatua ya kuomba ridhaa ya chama kuchaguliwa kuwa Spika ni hatua nzuri kwani kuwa na chaguzi nyingi inakuwa inatoa nafasi kupata mtu sahihi.

“Mimi ni Mbunge wa Jimbo la Hanang, wana  Hanang wameniamini, nikipata nafasi ya kuongoza Mhimili wa Bunge maana yake nitwaongoza wabunge wenzangu, ninavyo vigizo vyote vya kuwaongoza, nimekuwa kiongozi toka nikiwa mdogo, hekima na busara za kuongoza ninazo, Mimi najiona Kiongozi,” amesema Mhandisi Hhayuma.

Hata hivyo kwa mujibu wa ritaba ya Chama Cha Mapinduzi leo Januari 15 ndio mwisho wa uchukuaji na urejeshaji wa fomu za kuwania nafasi hiyo ya Spika ambayo kwa sasa iko wazi baada ya aliyekuwa  Spika Job Ndugai kuachia ngazi baada ya kuandika barua ya kujiuzulu,hivyo CCM ikatangaza mchakato wa kujaza nafasi hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...