Pamela Mollel,Dodoma


OFISA ardhi Mteule wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu Mkoani Arusha, Faraji Rushagama, amechukua fomu na kujitosa kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Akizungumza na wanahabari Mara baada ya kuchukua form hiyo Rushagama ambaye ni kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) amesema ni maono yake ya muda mrefu ya kutamani kuwatumikia wananchi

Amesema ameamua kutia nia kwa kuwa kiti hicho kipo wazi na katiba inampa fursa hiyo kwa mujibu wa ibara ya 82 ambapo Spika siyo lazima awe mbunge bali anaweza kuwa mwanachama wa chama chochote cha siasa.

“Nafikiri naona kabisa kwamba kwa sasa Spika ajaye anapaswa asiwe mbunge ili watanzania wapate ladha tofauti,” amesema Rushagama.

Amesema pamoja na kuwa na vigezo Nchi inahitaji kiongozi shupavu wa kuongoza mhimili wa kutunga sheria

Ofisa huyo wa serikali ambae kwa upande mwingine ni Mwanasheria amesema yeye anatokana na wananchi wa kawaida wasio wabunge hivyo anaamini atafanya vizuri zaidi kwa kuwa hataegemea upande wowote ambao unalenga ujimbo.

Alifafanua kuhusu wanaohoji kuwa yeye ni mdogo na Hana uzoefu amesema hayo ni Mambo ya kizamani kuwa kuwa bunge linaendeshwa kwa mujibu wa katiba na sheria na sio kwamba linabebwa mgongoni

"Nawashangaa Sana watu wanaohoji eti Mimi ni mdogo kwani ninakwenda kukubeba bunge kwamba litanielemea?

“Kikubwa sana hapa ni miongozo, kanuni na taratibu za uendeshaji kuzingatiwa lakini pia busara kwa maslahi ya watanzania zinapoonekana zipewe nafasi ,” amesema.

Kuhusu Sheria zinazolalamikiwa Mwanasheria huyo ameeleza kuwa sheria zikilalamikiwa ni kwamba wakati zinatungwa zilikuwa zinafaa ila kwa sasa kama hazifai atatoa ushauri na kufuata kanuni kwa serikali inayoleta miswaada Bungeni ili zitungwe sheria nzuri.

Je Rushagama ni nani? huyu ni wakili ambaye ni mzaliwa wa wilaya ya Karagwe mkoa wa Kagera, na kwa Sasa anafanya kazi Kama Ofisa ardhi Mteule wa Halmashauri ya wilaya ya Karatu

Elimu yake ana stashahada ya sheria kutoka chuo kikuu cha Tumaini Dar es Salaam, stashahada ya uzamili katika usuluhishi na upatanishi (ISW), Sheria kwa vitendo (LST) mutawaliwa.

Anayo pia shahada ya uzamili akibobea katika sheria za kimataifa na kazi kutoka Chuo kikuu Huria Tanzania (OUT) na anasomea sheria ya uzamivu katika sheria za kimataifa chuo kikuu ambacho hakukitaja.
Afisa Ardhi Mteule wa halmashauri ya wilaya ya Karatu Mkoani Arusha Faraji Rushagama jana amechukua fomu ya kuwania nafasi ya uspika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...